HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2024

Benki ya NMB yaipiga tafu Shule mbili za Sekondari mkoani Dar es Salaam, yakabidhi meza 90 na viti 90 vyenye thamani ya shilingi milioni 10

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda (katikati) akipokea sehemu ya msaada wa meza na viti 40 kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ferdinand Mpona (wa pili kulia) kwa ajili ya Shule ya Sekondari Uhamiaji iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhamiaji, Christopher Mtabutu, Meneja Mahusiano wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara (kushoto) na wa pili kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Kurasini, Jane Mubezi. (Na Mpiga Picha Wetu).   

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (wa pili kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa meza na viti 50 kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ferdinand Mpona (wa pili kulia) kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mchikichini. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mchikichini, Nelson Nestory na kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ilala, Christine Lifiga. (Na Mpiga Picha Wetu).

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (wa pili kushoto) akipmkabidhi sehemu ya msaada wa meza na viti 50 Mkuu wa Shule ya Sekondari Mchikichini, Nelson Nestory vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule hiyo. Katikati anayeshuhudia ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ferdinand Mpona, Diwani wa Kata hiyo, Azim Khan (kushoto) na kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Ilala, Christine Lifiga.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Benki ya NMB imekabidhi meza 90 na viti 90 venye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za sekondari mkoani Dar es Salaam, shule zilizokabidhiwa msaada huo ni Sekondari ya Uhamiaji iliyopo Wilaya ya Temeke  na Shule ya Sekondari Mchikichini ikiwa ni utekelezaji wa azma ya benki hiyo kuboresha elimu.

 

Samani hizo zitapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa madawati kwa walimu na wanafunzi na ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Uwekezaji kwa Kijamii (CSI) unaolenga kusaidia jamii ambapo benki hiyo inafanya kazi.

 

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi meza na viti hivyo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Ferdinand Mpona alisema uboreshaji wa sekta ya elimu ni miongoni mwa vipambule muhimu kwa benki yake huku alisisitiza dhamira ya benki hiyo kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wote ikiwemo Serikali katika kuinua maendeleo ya sekta ya elimu nchini kote.

 

"Kama benki, tunatambua kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha ndiyo maana kwa miaka mingi tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuinua ukuaji wa sekta ya elimu. Kwa hakika, sekta ya elimu ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika mkakati wetu wa CSI. Tumekuwa tukitenga asilimia moja ya Faida Baada ya Kodi (PAT) kila mwaka ili kuchangia mipango mbalimbali ya maendeleo,” alisema.

 

Mpona aliongeza, “Tunaamini samani tunazotoa leo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu,”

 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliipongeza benki hiyo kwa moyo wake wa ukarimu na kusisitiza dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ya kuendeleza maendeleo ya sekta ya elimu.

 

 “Tunafahamu kuwa shule nyingi za Wilaya ya Temeke bado zinakabiliwa na changamoto nyingi na zinahitaji msaada zaidi kutoka kwa wadau wa elimu kwa kuwa tuna bajeti ndogo. Naishukuru Benki ya NMB kwa kuunga mkono jambo hili zuri na nachukua fursa hii kutoa wito kwa wadau wengine wa ushirika kuungana na azma yetu ya kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu,” Mapunda alisema.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo wakati wa hafla ya kukabidhi meza 50 na viti 50 vilivyotolewa na benki ya NMB kwa Shule ya Sekondari Mchikichini alishukuru benki ya NMB kwa kuendelea kuunga juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu.

 

“Tunashikia faraja kwa benki yetu kwa kuendele kuwa karibu na wananchi. Mheshimiwa rais ameshaleta fedha za kujenga ghorofa katika shule hii ya Mchikichini na matundu ya vyoo. Kitendo cha benki ya NMB kutoa meza na vitu ni jitihada njema za kuunga mkono serikali na siku zote wamekuwa wakituunga mkono kwa vitendo,” alisema.

 

Awali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhamiaji, Christopher Mtabutu alibainisha kuwa shule yake ilikuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati ya walimu akionyesha matumaini kuwa madawati yaliyotolewa na benki ya NMB kwa kiasi kikubwa yatasaidia kukabiliana na upungufu huo.

 

“Mchango huu umekuja wakati muafaka kwani tumekuwa tukikabiliwa na upungufu wa madawati ya walimu. Ninaamini kuwa madawati na meza ambazo benki ya NMB imetupatia leo vivitasaidia tu kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu mbali na kuboresha usalama wa mali zao pia,” aliongeza.

 

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mchikichini Nelson Nestory alisema, “Msaada wa meza 50 na viti 50 utasaidia sana. Kabla ya kuomba msaada huu tulikuwa na upungufu wa meza na viti 150 na meza 50 ambapo Mkurugenzi alituletea viti 100 na meza 100. Tulikuw ba upungufu wa meza 50 na viti 50. Tunaishukuri benki ya NMB kwa kutupatia meza 50 na viti 50 na kwa sasa tumemaliza tatizo la wanafunzi kukosa meza na viti.


Aliahidi shule yake kuendelea kutunza msaada huo vyema ilikusaidia vizazi vijavyo.

No comments:

Post a Comment

Pages