HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 28, 2025

AICC na JNICC Yawapa Nafasi Watanzania na Wadau wa Kimataifa Kukodi Kumbi Zao

Na Miraji Msala 

KITUO cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) pamoja na Kituo cha Kimataifa cha 
Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), vimeendelea kuboresha huduma zao huku vikiwakaribisha Watanzania na wadau wa kimataifa kukodi kumbi zao kwa ajili ya mikutano, hafla na sherehe mbalimbali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 22 ya Wahandisi yaliyofanyika Mlimani City, Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa AICC, Bi. Mourine Kaaya, alisema kumbi hizo si kwa ajili ya mikutano ya kimataifa pekee, bali pia zinapatikana kwa sherehe mabalimbali hafla binafsi na mikutano ya ndani na ya nje.

“AICC imekuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa, lakini pia wananchi wa Dar es Salaam na Arusha wamenufaika kupitia wageni wanaokuja kwenye kumbi hizi kwa kuwa wanahitaji huduma za malazi, usafiri na chakula. Hii ni hatua kubwa kwa taifa kwa ujumla,” alisema Kaaya.

Aliongeza kuwa AICC na JNICC zimekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza mapato kupitia sekta ya mikutano na utalii, huku zikiendelea kutoa nafasi kwa wananchi na wadau binafsi kukodi kumbi kwa gharama nafuu kulingana na mahitaji yao.

“AICC na JNICC si za mikutano pekee, tunazo kumbi ndogo ndogo zinazotumika kwa hafla za kijamii. Tunawakaribisha wadau wote kuendelea kutumia huduma hizi kwa sababu ni sehemu ya kuchangia maendeleo ya taifa letu,” alisisitiza.

Kwa mujibu wa Kaaya, kumbi hizo zimeendelea kuvutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi, hatua inayochochea ukuaji wa uchumi wa maeneo jirani kupitia sekta ya huduma.



No comments:

Post a Comment

Pages