LICHA ya kucheza kandanda la kiwango cha chini, lisilo na mvuto kwa mashabiki, Mabingwa wa Tanzania, Young Africans 'Yanga,' wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wiliete Benguela SC ya Angola na hivyo kufuzu raundi inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL 2025/26).

Yanga walikuwa wenyeji wa mechi hiyo ya marejeano kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ilikoingia ikiwa na uongozi wa mabao 3-0 iliyoupata katika mechi ya kwanza dimbani Novemba 11 (11 de Novembro) jijini Luanda, nchini Angola wiki iliyopita.
Tofauti na mechi ya awali ambako walishinda kirahisi, Yanga iliwalazimu kusubiri hadi dakika ya 70 kupata bao la uongozi lililowekwa kimiani na Pacome Zouzoua, akimalizia gonga zake maridadi na straika 'mwili jumba' Andy Boyeli, aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Prince Mpumelelo Dube.
Bao la pili la Wana Jangwani limefungwa na kiungo mkabaji Azizi Andabwile kwa kichwa akiunganisha Kona ya Offen Chikola, hivyo kuipa Yanga ushindi wa ujumla wa mabao 5-0 dhidi ya Wiliete Benguela SC na sasa wanataumana na Silver Strikers ya Malawi, ambayo imewatupa nje Association Sportive Elgeco Plus (ASSM Elgeco Plus) ya Madagascar.
Katika mechi iliyochezwa leo, Silver Strikers FC ikiwa nyumbani imevuna sare tasa dhidi ya ASSM Elgeco Plus, wiki moja tangu walipomaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1, jijini Antananarivo, nchini Madagascar, hivyo kufuzu raundi ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini.

Yanga wanaonolewa na Mfaransa Romain Folz, wataanzia ugenini nchini Malawi kati ya Oktoba 17 na 19, kisha marudiano kupigwa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kati ya Oktoba 24 na 26 na mshindi wa ujumla atafuzu hatua ya makundi CAF CL 2025/26.
September 28, 2025
Home
Unlabelled
Yanga yatakata CAF CL, tiketi ya Makundi iko kwa Wamalawi
Yanga yatakata CAF CL, tiketi ya Makundi iko kwa Wamalawi
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment