DENIS MLOWE IRINGA
BAADA ya kimya cha Muda Fainali ya mashindano ya kombe la Vunjabei 2025 itachezwa leo kati ya Kising’a fc dhidi ya Mgela Fc.
Mchezo
huo utapigwa katika uwanja wa shule ya msingi Mlandege ambapo kabla ya
mchezo huo kutakuwa na mchezo wa utangulizi kati ya timu ya Chama cha
Mpira dhidi ya timu ya jeshi la Polisi.
Akizungumza
na mwandishi , Katibu wa mashindano hayo, Pastor Kwambiana alisema kuwa
licha ya Fainali hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali hili kuweza
kuifanya iwe na mvuto zaidi na kuwataka mashabiki wa soka kufika kwa
wingi kushuhudia mchezo huo.
"Shughuli
itapambwa na matukio/burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchezo wa
utangulizi utakao husisha timu ya CHAMA CHA MPIRA dhidi ya timu ya JESHI
LA POLISI." Alisema
Aliongeza kuwa Mchezo
utakaoanza majira ya saa nane kamili mchana na baadaye majira ya saa
kumi kamili jioni utachezwa mchezo wa fainali hiyo kati ya KISING'A FC
dhidi ya MGERA FC.
Hivyo wapenzi, wadau,
mashabiki na watazamaji wa michezo mnakaribishwa sana kuja kushuhudia
nani ataibuka na milioni 10 zilizoko mezani kwa ajili ya bingwa na
kudhaminiwa na mkurugenzi wa kampuni ya VunjaBei Fred Ngajilo.
Mshindi wa pili ataibuka na kiasi cha sh milioni 3 na mshindi wa 3 ataondoka na milioni 2.
Aidha
alisema kuwa kutakuwa na zawadi kwa mchezaji bora wa mashindano,timu
yenye nidhamu, mwandishi bora katika vipengele vitano kama
tv,blog,gazeti, mitandao na radio.




No comments:
Post a Comment