KIKICHEZA kwa mara ya kwanza tangu kilipoachana na Kocha Mkuu Fadlu Davids, kikosi cha Simba SC kimeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate FC, katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, matokeo yaliyowawezesha kuwashusha mabingwa watetezi Yanga kunako msimamo wa ligi hiyo.

Saa 24 kabla, Yanga waliwachapa Pamba Jiji FC ’Wana TP Lindanda' kwa mabao 3-0 na kukaa kwenye nafasi ya nne ya msimamo wa NBC PL 2025/26, lakini ushindi wa Mnyama umewashusha Yanga hadi nafasi ya tano, huku Simba ikikalia nafasi ya nne kwa faida ya mpangilio wa alfabeti za kwanza za majina ya timu hizo.
Wekundu wa Msimbazi kwa sasa wako chini ya Suleiman Matola (kwa mechi za ndani), huku Hemed Suleiman 'Morocco' akitangazwa kuwa Kocha wa Muda 'caretaker' kwa mechi za kimataifa na matokeo hayo yanamaanisha kuwa tayari Matola amefanya jukumu lake vema, huku Morocco akitarajia kuingia mzigoni Jumapili hii wanaporudiana na Gaborone Utd ya Botswana.

Mfungaji Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Jean Charles Ahoua, ndiye aliyeibuka shujaa wa dakika 45 za kwanza, baada ya kutoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Rushine de Reuck, kisha kufunga bao la pili na kuwapeleka mapumziko na uongozi huo, unaofungua ukurasa mpya wa msimu mpya wa 2025/26.
Katika kipindi cha pili, 'Simba Mweusi' Jonathan Sowah aliifungia Simba bao la tatu na la mwisho, alipokuwa akiunganisha krosi maridadi ya Elie Mpanzu Kibisawala, kukamilisha ushindi mnono unaofanana na ule wa kwanza msimu uliopita walipowaalika Tabora United (ambayo kwa sasa inatambulika kama TRA United FC).
September 26, 2025
Home
Unlabelled
Simba yaifumua Fountain Gate, yaishusha Yanga
Simba yaifumua Fountain Gate, yaishusha Yanga
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.




No comments:
Post a Comment