HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 20, 2025

HT: Gaborone Utd 0-1 Simba SC

DAKIKA 45 za kwanza za pambano raundi ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL 2025/26 - preliminary round), kati ya Gaborone United ya Gaborone, Botswana, zimekamilika kwa Wekundu wa Msimbazi kuongoza kwa bao 1-0.

‎Simba wametawala dakika 45 hizo za kwanza kwenye dimba la Obedi Itani Chilume, walikonufaishwa na bao la Elie Mpanzu Kibisawala, kunako dakika ya 16, kwa kichwa akiunganisha kimiani krosi ya nahodha Shomari Kapombe.

‎Licha ya zaidi ya nusu kikosi kujumuisha nyota wapya, Simba wameoneaha uhatari uliowapa uongozi huo muhimu kwa Wekundu hao wa Msimbazi, kuelekea kushinda mechi hiyo na kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo. 

‎Simba inayonolewa na kocha Fadlu Davis, anayedaiwa kujiandaa kuipa mkono wa kwaheri, iko dimbani ikiwa na nyota wapya saba, aliwemo Anthony Mligo, Allasane Kante, Rushine de Reuck, Naby Camara, Neo Maema na Suleiman Mwalimu.


No comments:

Post a Comment

Pages