KIKICHEZA kwa mara ya kwanza bila Kocha Mkuu wake Fadlu Davids, kikosi cha Simba SC kimechanga vema karata zao katika dakika 45 za awali za mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, inakoongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate FC ya Manyara hadi mapumziko.

Wekundu wa Msimbazi wanaoongozwa kwa muda na Hemed Suleiman 'Morocco' anayesaidiwa na Suleiman Matola, wametawala dakika 45 za kwanza za mtifuano huo kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na huenda ingepata mabao zaidi kama nyota wake wangekuwa makini katika boksi la wapinzani.
Mfungaji Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Jean Charles Ahoua, ndiye aliyeibuka shujaa wa dakika 45 za kwanza, baada ya kutoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Rushine de Reuck, kisha kufunga bao la pili na kuwapeleka mapumziko na uongozi huo, unaofungua ukurasa mpya wa msimu mpya wa 2025/26.
September 25, 2025
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.





No comments:
Post a Comment