HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 25, 2025

Mkuu wa Majeshi ampandisha cheo Alphonce Simbu ‎

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda, amempongeza Mwanariadha Mtanzania na askari wa Jeshi hilo, Alphonce Simbu, kwa kutwaa medali ya dhahabu ya mbio ndefu (Marathon) za Mashindano ya Dunia (WAC 2025), yaliyofanyika Tokyo, nchini Japan.

‎Simbu aliibuka na ushindi huo mwishoni mwa kinyang'anyiro hicho, akikimbia kwa masaa mawili, dakika tisa na sekunde 48 (2:09:48) na kumpiku nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Amanal Petros kwa sekunde sifuri nukta tatu (0.03), huku Iliass Aouani wa Italia akimaliza wa tatu akikimbia kwa masaa mawili, dakika tisa na sekunde 53 (2:09:53).

‎Baada ya kurejea nchini juzi, CDF Mkunda leo amelutana na nyota huyo, ambako licha ya pongezi hizo, Jenerali huyo amempandisha cheo kutoka Sajini, na sasa kuwa Sajinitaji, wakati wa hafla  iliyofanyika Makao Makuu ya Ulinzi (JWTZ), yaliyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.

‎Jenerali Mkunda amesema ushindi wa Simbu ni wa Watanzania wote na Afrika kwa ujumla na kwamba michezo ni sehemu ya kazi jeshini, hivyo Sajinitaji Simbu amefanya kazi nzuri, huku akiwataka maafisa na askari wote jeshini kuiga mfano wa Simbu kwa kufanya kazi kwa bidii na kuleta mafanikio katika kila idara jeshini. 


No comments:

Post a Comment

Pages