HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 24, 2025

Mbeto: Ni Zanzibar pekee Afrika wazee wote wanalipwa posho kila mwezi

Mwandishi Wetu, Zanzibar

Awamu ya nane chini ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na mgombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao 29 Oktoba 2025, ndio serikali pekee Afrika ambako wazee wote waliofikisha umri wa miaka 70 wanalipwa posho bila kujali iwapo ana pensheni ya kustaafu au la.

Akizungumza na wanahabari, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema kwenye masuala ya ustawi wa jamii, Rais Dkt. Mwinyi amefanya mambo makubwa kuliko kiongozi yoyote, Afrika.

Alisema awali waliofikisha miaka 70 waliopo mitaani na katika nyumba za kutunzia wazee wanalipwa TSh.40,000 kila mwezi na pesa hizo ni tofauti na TSh.50,000 ya pensheni kwa wastaafu ambayo awali ilikuwa TSh.20,000.

"Ukikuta mtu huyo alikuwa mtumishi wa umma na sasa kastaafu anakula 90,000 kwa mwezi" alisema Mbeto.

Alibainisha kuwa mzee kama huyo kama anayeishi nyumba za kulelea wazee za Sebuleni, Limbani Pemba na Welezo anakuwa na nafuu ya maisha maradufu maana kila kitu anapata  bure katika nyumba hizo.

Alisema katika nyumba hizo chakula, mavazi, maji, umeme, matibabu bure na pia Sera ya Taifa kuhusu wazee inasisitiza kupewa vipaumbele kwenye huduma za jamii.

"Hilo ACT hawalisemi katika mikutano yao wala hawaelezi watafanyia nini waZanzibari zaidi ya kuzungumzia Muungano na kutoa maneno ya chuki na ubaguzi" alisema Mbeto.

Alibainisha kuwa Dkt. Mwinyi pia ameagiza kupitia Wizara ya Kazi kuhakikisha, mshahara kima cha chini isipungue 350,000 na michango yote lazima iwasilishwe mifuko ya hifadhi na fao la uzazi na dharula mfanyakazi anapopata janga la moto au mafuriko ni mambo ambayo lazima atimiziwe mwajiriwa iwe sekta binafsi au serikalini.

Mbeto ametaka Dkt. Mwinyi apewe kura nyingi ili ashinde kwa kishindo kikubwa ili kuondoa nongwa za kina Othman Masoud Othman 'OMO' na kundi lake la ACT ambalo alibainisha kuwa linaenda kusambaratika baada ya uchaguzi.


 

No comments:

Post a Comment

Pages