Na Miraji Msala
Mgombea udiwani wa Kata ya Goba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lawrence Mlaki, ameahidi kutekeleza miradi ya kipaumbele ikiwemo ujenzi wa barabara, upatikanaji wa maji na maboresho ya michezo endapo atapewa ridhaa ya kuendelea kuongoza.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Kwa Madawa, Mlaki alisema ujenzi wa barabara ya Mkorea kwa kiwango cha lami utaanza ndani ya siku kumi zijazo na kuomba ushirikiano wa wananchi. Aliongeza kuwa baada ya kukamilika, atashirikiana na Mamlaka ya Usafiri wa Dar es Salaam (LATRA) ili kuhakikisha huduma za daladala zinapatikana.
“Kwa kushirikiana na wananchi, tayari kituo cha polisi kimekamilika. Hii ni hatua muhimu kwa usalama wetu sote,” alisema Mlaki huku akitoa shukrani kwa mshikamano wa wananchi.
Akizungumzia changamoto ya maji, Mlaki alisema mgao umekuwa mkubwa na mabomba yaliyosambazwa hayajafanyiwa kazi ipasavyo, hivyo atahakikisha tatizo hilo linapatiwa suluhu. Vilevile, alieleza kuwa eneo la soko tayari limetengwa na atasimamia utekelezaji wake.
Aidha, Mlaki aliahidi kushirikiana na wawekezaji kuboresha uwanja wa Nike kwa ajili ya kukuza michezo kwa vijana.
“Naomba wananchi mtupatie kura kuanzia kwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge na udiwani, ili tuweze kusimamia maendeleo ya kata yetu kwa uhakika,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Goba, Londisomni Chikaka, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuichagua CCM kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani. Alisema wagombea wa vyama vingine ni “wapiga kelele wasioweza kuleta maendeleo,” na kusisitiza wananchi wasifanye makosa kwenye siku ya kura.
September 23, 2025
Home
Unlabelled
Mgombea Udiwani Mlaki Aahidi Kuboresha Miundombinu Goba
Mgombea Udiwani Mlaki Aahidi Kuboresha Miundombinu Goba
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.




No comments:
Post a Comment