DENIS MLOWE, IRINGA
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Iringa Mjini, Frank Nyalusi amefariki dunia usiku wa kumkia leo katika Hospital ya Rufaa Mkoa wa Iringa.
Nyalusi aliyekuwa akiumwa kwa kipindi cha miezi kadhaa taarifa yake imetolewa mapema asubuhi ya leo ikisema kwamba
'Kwa masikitiko makubwa tunapenda kutoa taarifa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa M/Kiti Frank John Nyalusi kwamba amefariki usiku wa leo.
Mwenyezi Mungu akampe pumziko la Milele.
Akawe mfariji kwa familia, Ndugu, jamaa na marafiki na wanachama wote wa CHADEMA.
Tunamshukuru Mungu kwa maisha yake hapa duniani
Nyuma yetu mbele yake
Hakika Vita umevipiga na mwendo umeumaliza tutaonana baadae kaka wa wote"
Katika hali ya huzuni zaidi kwa familia ya Nyalusi wiki mbili zilizopita Nyalusi alifiwa na mama yake mzazi ghafla mara baada ya kumwona kijana wake akiwa katika hali mbaya ya kuumwa alipokuwa amelazwa katika Hospital ya Wenda.
September 19, 2025
Home
Unlabelled
MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA IRINGA MJINI AFARIKI DUNIA
MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA IRINGA MJINI AFARIKI DUNIA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.




No comments:
Post a Comment