DAR ES SALAAM, TANZANIA
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeainisha mafanikio ya utekelezaji wa majukumu iliyopata katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ikiwemo ujenzi wa maabara katika Mikoa ya Kimkakati ya Dodoma na Mwanza, utakaogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 36.8.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk. Ashura Katunzi, wakati wa mkutano wake na Wahariri na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali, alikofafanua kuwa ujenzi huo na maboresho ya ofisi zingine za Kanda, Bandari na Mipakani, unalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ukaribu na kupunguza gharama.
Dk. Katunzi alibainisha ya kwamba, Ujenzi wa Maabara za mkoani Dodoma utagharimu kiasi cha Sh. Bilioni 24.7, huku ule wa mkoani Mwanza ukitarajiwa kugharimu zaidi ya Sh. Bil. 12 na kwamba maabara za Dodoma zitahudumia mikoa mitatu ya Kanda ya Kati na zile za Mwanza zitahudumia Mikoa sita ya Kanda ya Ziwa.
“Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ukaribu na kupunguza gharama, Serikali kupitia TBS imeanza ujenzi wa maabara katika mikoa ya kimkakati ya Dodoma na Mwanza. Ujenzi wa maabara hizi utagharimu jumla ya kiasi cha Sh. 36,802,360,422.39, sawa na Sh. 24,723,478,765.48 kwa Dodoma na Sh. 12,078,881,656.91 kwa Mwanza.
“Kwa upande wa Dodoma, maabara zitakazojengwa zitahudumia mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora pamoja na mikoa mingine ya karibu, huku maabara za Mwanza zikitarajiwa kuhudumia mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu,” alisema Dk. Katunzi wakati wa mkutano huo jijini Dar es Salaam leo Septemba 18.
Ukiondoa kusogeza Huduma Karibu kwa Wateja, Dk. Katunzi alibainisha maeneo mengine ambayo shirika lake limepata mafanikio makubwa kuwa ni pamoja na; Kuwezesha Biashara, Kuongeza Ufanisi wa Maabara, Kuimarisha Mifumo ya TEHAMA- ICTM, Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, pamoja na Tuzo na Umahiri.
Dk Katunzi alisema mwaka 2023, TBS ilishinda Tuzo ya kuwa Mdhibiti Bora Barani Afrika, tuzo aliyosema inaakisi dhamira ya TBS katika utendaji bora na mchango wake chanya katika kukuza viwango na kudhibiti ubora wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi na zile zinazoingizwa kutoka nje.
“Vilevile, TBS imekuwa taasisi ya kwanza katika Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kupata Ithibati (accreditation) ya Mifumo ya Udhibiti Ubora wa Bidhaa (Product Certification) ya kimataifa katika wigo mpana (wide scope) ndani ya muda mfupi na ni ya taasisi ya tatu kupata ithibati hiyo iliyotolewa na SADCAS Septemba, 2024.
“Pia kwa mwaka 2025, TBS imefanikiwa kupata Ithibati ya Umahiri wa Mfumo wa Usimamizi wa Chakula katika kiwango cha kimataifa toleo jipya (ISO 22003:2022), ambapo kuhamia kwenye Ithibati hii kunaifanya TBS kuwa taasisi ya kwanza katika nchi za SADC kupiga hatua hiyo,” alisema Dk. Katunzi.
Katika Kuwezesha Biashara, Dk. Katunzi alisema TBS ina Kamati za Kitaalam (Technical Commitees) za Uandaaji Viwango 115 katika sekta ya chakula, kemikali, uhandisi mitambo, uhandisi umeme, uhandisi ujenzi, nguo na ngozi, madini na mitambo ya uchimbaji madini, mazingira na mtambuka (general tecniques).
“Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, TBS imefanikiwa kuandaa viwango 2,765 vya sekta mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya soko ambavyo vitasaidia wafanyabiashara, wajasiriamali na watoa huduma kuzalisha bidhaa bora zenye kukidhi matakwa ya viwango, hivyo kuwawezesha kufanya biashara ndani na nje ya nchi.
“Aidha, jumla ya vyeti na leseni za ubora 3,184 vimetolewa kwa wazalishaji, miongoni mwao wakiwemo wajasiriamali wadogo 1,359, ambako Serikali kupitia TBS imekuwa ikitenga zaidi ya Sh. Mil. 350 kila mwaka kwa madhumuni ya kuhudumia wajasiriamali wadogo bila ya malipo yoyote,” alifafanua Dk. Katunzi.
September 18, 2025
Home
Unlabelled
TBS yaanika mafanikio yake, yaanza ujenzi wa Maabara za Bil. 36.8/- Dodoma, Mwanza
TBS yaanika mafanikio yake, yaanza ujenzi wa Maabara za Bil. 36.8/- Dodoma, Mwanza
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.


No comments:
Post a Comment