NA DENIS MLOWE, IRINGA
BENKI
Azania Tawi la Iringa imeadhimisha wiki ya huduma kwa mteja lengo kuu
likiwa ni kuwashukuru wateja wake kwa kuwa nao bega kwa bega katika
ukuaji wa benki hiyo mkoani hapa.
Maadhimisho
hayo yaliyofika kelele leo na mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Iringa
Kheri James aliyeambatana na wateja mbalimbali wa benki hiyo.
Akizungumza
wakati wa kuhitimisha maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa , Kheri
James aliwataka wajasiriamalii kuepuka wakopeshaji vishoka maarufu kama
kausha damu na kutumia benki hiyo kwa kutokana na riba ndogo na uaminifu
kujiletea maendeleo.
Alisema
kuwa wananchi na wajasiriamali mkoani hapa watumie huduma za kibenki
zilizo kwa wingi kuepukana na unyonyaji unaofanywa na watu wasio na nia
njema kwao mwisho wa siku wanalizwa.
“Najua
fika kwamba kusogezewa karibu huduma za kifedha ikiwemo uwingi wa benki
mkoani hapa ni fursa kubwa kiuchumi hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kutumia
ipasavyo uwepo wa huduma hizi kwa wananchi " Alisema
Aliongeza
kuwa kutumia vema uwepo wa benki kama hii ya Azania kwa kutunza akiba
zenu na pia kukopa ili kuwekeza na kukuza biashara zenu itasaidia kukua
kwa uchumi wa kila mmoja na taifa kwa ujumla.
Hata
hivyo Kheri James alitoa rai kwa benki hiyo kuendelea kubuni mipango
mbalimbali ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia benki
sambamba na kubuni huduma zinazowagusa wananchi wa wenye hali ya kawaida
kiuchumi ili waweze kutumia vema fursa na huduma zinazotolewa na benki
hiyo. Hususani katika mikopo
Alisema kuwa
katika kutoa elimu hiyo angalieni fursa ambazo zinapatikana kwa wingi
mkoani hapa kama vile ujenzi wa hotel kubwa ambazo zinaweza chukua watu
hata 1000 kwa siku, kumbi ambazo zinaweza beba watu 2000 na sehemu
nyingi ukigusa zinafursa hivyo jukumu la benki kutoa mikopo kwa
kuangalia fursa kama hizo.
Kwa upande wake
Meneja wa Benki hiyo tawi la Iringa, Gaile Lungwa alisema kuwa hiyo
inamilikiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo NSSF PSSSF,NHIF
wamejipanga kutoa huduma bora kwa wateja na zenye riba nafuu hivyo wana
wajibu mkubwa wa kusaidiana na serikali katika kuendeleza umma wa
watanzania.
Alisema kuwa benki ya Azania
imeelekeza nguvu zake katika kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora
kulingana na mahitaji yake na wanahudumia aina zote za wateja wakiwemo
wakulima na wafugaji
Alisema kuwa mwaka huu
benki ya Azania wamekuja na kauli mbiu inayosema Ni Mission Possible
hivyo wamefanikiwa kuwafikia wateja katika wilaya zote za mkoa wa Iringa
na kama Azania wamejikita katika huduma za akaunti mbalimbali, mikopo
ya aina mbalimbali hususani ya kilimo na ufugaji
Vile vile
alisema kuwa wana mikopo ya wakina mama yenye riba nafuu ya asilimia
moja kwa mwezi lakiini pia wana mikopo ya wastaafu yenye riba ndogo
sana kwa kuamini kwamba ukistaafu bado una fursa ya kuendelea kufanikiwa
.
Aidha aliongeza kuwa tangu
kufunguliwa kwake Aprili 4 mwaka huu Azania tawi la Iringa wamefanikiwa
kutoa mikopo ya zaidi ya bilioni 3 kwa kipindi cha miezi 6 na
wanufaikaji wengi wamekuwa wakinamama,wafanyakazi ,wakulima
wafugaji,wastaafu, vijana na makundi mengine mkoani hapa.




No comments:
Post a Comment