HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 14, 2025

Mbeto awatoa hofu wapiga kura

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Wananchi wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametakiwa kutokuwa na hofu, uchaguzi utakuwa huru, amani na wa haki.

Akizungumza na wanahabari Unguja 13 Oktoba 2025, Katibu wa Kamati ya Maalum ya NEC, Zanzibar Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema hadi hivi sasa hakuna taarifa zozote za matukio ya uvunjifu wa amani wala kitu kingine cha namna hiyo hali ambayo ni njema na ina ashiria amani na utulivu.

Mbeto alisema waTanzania ni waelewa ndio maana kumekuwa na utulivu.

Alisema hali hiyo inachangiwa na ahadi za CCM zilizopo kwenye Ilani ya chama hicho, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano kwa ujumla kutelelezwa kikamilifu.

Alibainisha kuwa vyama vinafanya kampeni zake kwa uhuru na kuhusiana na suala la katiba mpya aliwashangaa ACT na Chadema.

Alisema mabadiliko ya katiba ni mchakato na ilichofanya serikali ni mabadiliko madogo ya sheria namba 2 ya 2024 Ibara ya 74 inataja Tume Huru ya Uchaguzi na Ibara ya 28 inasema tume iliyopo itakoma muda wake ifikapo 2027 itakapokuwa imekamilisha uchaguzi mkuu.

"Kifungu a, b, c kinaeleza kuwa watachaguliwa wajumbe wa tume wenye sifa zilizoainishwa" alisema na kubainisha kuwa huo si mchakato wa siku moja.

"Baadhi ya vyama hususan ACT Wazalendo na Chadema visubiri 2030 itakapopatikana na marekebisho mengine" alisema.

Alibainisha kuwa Chadema awali walipigia kelele katiba mpya, mara Tume Huru ya Uchaguzi lakini 2015 wanasahau wakiwa wameungana na kujiita Ukawa na kumsimamisha kuwania kuwa Edward Lowassa (marehemu) kugombea kuwa  Rais alipata asilimia 45 hadi 46 ya kura zote.

"Waliongoza halmshauri karibu zote za miji mikubwa mameya wakitoka vyama vyao, wakapata wabunge wengi nchi nzima mbona ilikuwa tume hii wasiyoitaka, ukisema hakuna demokrasia, tume sio huru sio kweli, mbona iliwatangaza?" alihoji Mbeto.

Mwenezi huyo alisema, Chadema ilijichanganya yenyewe kwa kuitisha uchaguzi wa mwenyekiti wa chama chao kipindi cha karibu na uchaguzi mkuu 2025.

"Kulikuwa na kambi ya Mbowe yenye nguvu na ya Lissu na CCM mara nyingi chaguzi hizo huwa tunafanya mapema hata yakitokea makovu tunapata muda wa kuyarekebisha.


No comments:

Post a Comment

Pages