HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 24, 2025

MSOWOYA, MSAMBATAVANGU WANENA MAZITO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29

DENIS MLOWE, IRINGA


MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Iringa Dk Tumaini Msowoya amewashauri Watanzania wasikubali kudanganyika badala yake waitunze amani ambayo Tanzania imetunukiwa.

Amesema wanaohamasisha maandamano na kutopiga kura wengi wapo wakiwa nje ya nchi hivyo huenda hawana uchungu wowote hata yakitokea machafuko.

Msowoya alikuwa akizungumza katika Mkutano wa Kufunga Kampeni za Jimbo la Iringa Mjini uliofanyika viwanja vya Kihesa.

"Ndugu zangu hatuna Tanzania nyingine, hapa ndio nyumbani. Hao wanao hamasisha maandamano na kutopiga kura hawapo Tanzania. Tusidanganyike," amesema.


Msowoya alitumia nafasi hiyo kuomba kura za Rais Dk Samia Suluhu Hassan, mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, mgombea Ubunge wa Iringa Mjini, Fadhir Ngajiro na Madiwani.

"Kuhusu kazi za Rais Samia hatuna mashaka, amefanya kazi kubwa na ya kutukika, zawadi yetu kwake ni kura za kutosha tarehe 29," amesema Dk Msowoya.

Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Iringa mjini, Jesca Msambatavangu amewataka wananchi mkoani hapa wasidanganyike na kauli za baadhi ya watu wasioitakia mema nchi.


Alisema kuwa maendeleo yaliyofanywa na serikali ya Mama Samia yameonekana na kila mmoja na miradi ya maendeleo inayoendelea ni kwa vizazi vijavyo na Gen Z wa sasa hivyo wasithubutu kufanya kinyume na sheria kwani jahaz likizama ni ngumu kuinuka

Msambatavangu alisema kuwa katika suala la ni CCM pekee imeanza kuyaleta tangu tunapata uhuru na amani iliyopo ni kutokana na uangalizi mzuri wa serikal iliyochini ya chama hiki.

"Nawaomba sana Gen Z  tusonge mbele na ikifika 29 tukapige kura watoto wetu wanahitaji maendeleo ni kwa ajili yao  na maendeleo hayo yataletwa na CCM " Alisema


Aliongeza kuwa asiwashawishi mtu kwenda kufanya ujinga wowote na kuzama kwenye vurugu kwani miradi ya maendeleo mmeona ikifanyika kwa wazi kabisa , vituo vya afya vimejengwa, shule zimejengwa, miundo mbinu ndio usiseme.




No comments:

Post a Comment

Pages