HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 09, 2025

Dkt. Mwinyi aahidi ajira zaidi kwa vijana

Na Mwandishi Wetu, Pemba

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kutoa ajira nyingi zaidi kwa vijana katika serikali atakayounda iwapo atashinda katika uchaguzi mkuu, ujao unaotarajiwa kufanyika, 29 Oktoba 2025.

Dkt. Mwinyi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akizungumza na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Wawakilishi Wete, mkoa wa Kaskazini Pemba, alisema uzoefu alioupata kaika kipindi cha miaka mitano ya alichokuwa madarakani amebaini kuwa vijana ukiwapa madaraka wanatekeleza vizuri.


"Ahadi yangu Mwenyezi Mungu akitujaalia nikarudi madarakani tutachukua vijana wengi serikalini" alisema.

Mgombea huyo alisema hana wasiwasi na ushindi kwa sababu yote waliyoahidi wametekeleza.

Sababu ya pili alibainisha kuwa ni kutokana na kupata uungwaji mkubwa mkono na vijana.

"Ukiwa na vijana kama hawa unashindwaje?"alisema na kuongeza kuwa ukiona Rais anacheza Singeli, ujue CCM raha"


No comments:

Post a Comment

Pages