HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2025

Mbeto: ACT kina Sera hatari za ukabila na Ubaguzi

Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  kimesema ACT Wazalendo kina   ajenda ya siri na sera za ubaguzi hivyo ni hatari kwa mustakabali  wa amani ya  Zanzibar na watu wake ikiwa siku kitapata bahati kikachaguliwa kushika dola.

Mbeto alisema hayo kufuatia hatua ya Makamu   Mwenyekiti wake Ismail Jussa Ladhu,  kumshambulia jukwaani mgombea Urais  wa CCM, Rais Dk  Hussein Ali Mwinyi akidai  hana asili ya Zanzibar ni ushahidi tosha ACT si chama sahihi kwa mustakbari mwema wa Zanzibar.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum  ya NEC Zanzibar,  Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis , aliyesema  ACT kina Sera za  kibaguzi na ubaguzi ni hatari  kwa ustawi wa umoja na mshikamano wa Kitaifa. 

Mbeto alisema karibu wananchi wote wa Zanzibar aidha watakuwa na asili moja  ya Zanzibar na nchi nyingine.

Katika moja ya mikutano ya kampeni za uchaguzi hivi karibuni wa ACT, Jussa alidai kuwa chama chake kikishinda Urais,  watu wasio na asili ya Zanzibar  watarudishwa kwenye asili zao na kudai mmojawapo ni Rais Dkt. Hussein Mwinyi ambaye alidai kwao ni Mkuranga, mkoa wa Pwani, Tanzania Bara.

Mbeto alisema huo ni ubaguzi mpya ambao hautoi taswira njema kwa Zanzibar.

Akitoa mfano alisema kwa Zanzibar ni kisiwa cha watu wenye asili mchanganyiko na rangi mbalimbali (Cosmopolitans), hivyo atawaondoa watu wangapi na kuwaacha wangapi.

"Jussa amekuwa akimnyooshea kidole Rais Dk Mwinyi na kudai ana asili ya Mkuranga Tanzania Bara. Cha ajabu Jussa  hataji asili yake ambayo ni India?" alihoji Mbeto.

Alisema kuwa mtu mwenye asili ya Mkuranga na India yupi aliyetoka nje ya Bara la Afrika.

Aidha alisema katika dunia ya sasa ambayo muafrika amezaa na mJapani, kuna  waChina na Mgoa   waliozaliwa Zanzibar na mtu  mwenye  asili ya Rwanda na Malawi amekuwa Rais wa Kwanza  Zanzibar, madai ya Jussa ni zaidi ya upuuzi. 

"Zama ya ubaguzi wa rangi asili na ukabila imekwisha duniani. Kiongozi anayebagua wenzake  kwa rangi, kabila  au asili ni katili kuliko kiongozi wa zamani Afrika  Kusini Pick Botter " alieleza.

Mbeto alidai  Jussa ni mwanasiasa  aliyeshindwa  kujenga hoja za kisiasa na sasa anahubiri ubaguzi. 

'Hutamsikia hata siku moja akinadi sera za chama chake jukwaani anachokijua  ni mtamko ya ubaguzi, wivu na chuki binafsi " alisema katibu mwenezi huyo. 


No comments:

Post a Comment

Pages