HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 03, 2025

Dkt. Mwinyi: Bilioni. 61 zimetengwa fidia Mangapwani

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Jumla ya Tsh.Bilioni 61 zimetengwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  (SMZ) kwa ajili ya fidia kwa watakaopisha ujenzi wa bandari jumuishi ya Mangapwani, mkoa wa Kaskazini, Unguja.

"Fidia hiyo ni kwa wale ambao watataka kulipwa pesa lakini pia ujenzi wa nyumba 54 za kisasa zimekamilika kwa watakaotaka nyumba badala ya pesa" alisema.

Alisema nyumba zilizojengwa serikali imejitahidi ziwe na hadhi kuliko walizotoka.

Mgombea huyo kwa tiketi ya  CCM alisema Mangapwani ni kijiji cha bandari kwani kunajengwa   sehemu ya meli kushushia mafuta,  nafaka na  chelezo cha kutengenezea meli. 

Miundombinu ya barabara imekamiliki baadhi ya maeneo sanjari na madaraja.

Aliwataka wananchi wa Bumbwini kuilinda amani ili maendeleo zaidi yaweze kupatikana.

Upande mwingine mgombea huyo alisema maboresho yaliyofanywa kwenye sekta ya elimu ufaulu umepanda na akipewa ridhaa anataka ufaulu uwe kwenye daraja la kwanza na la pili na wote wenye sifa wataenda vyuo vya elimu ya juu.

Mkoa wa Kaskazini una shule sita za ghorofa zenye maabara za kisasa, maktaba na madarasa ya kompyuta.


 

No comments:

Post a Comment

Pages