Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutunza tunu za Taifa.
Akizungumza na wanahabari Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Zanzibar Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema tunu za Taifa ni amani na umoja wetu.
" Tutunze tunu za Taifa letu tulizoachiwa na Baba wa Taifa, uchaguzi huja kila baada ya miaka mitano" alisema Mbeto.
Alibainisha kuwa uchaguzi usilitoe Taifa kwenye misingi ya kulienzi kwani likiparaganyika waTanzania hawana pa kukimbilia.
^Hakuna atakayesema atakimbilia kwa mjomba akakae " alisema Mbeto na kutaka wakati ukifika wenye sifa wajitokeze wakapige kura.
Mwenezi Mbeto alitaka Baba wa Taifa aenziwe kwa kukemewa kwa vitendo vya rushwa, uhujumu uchumi, ubadhirifu kwani vyote hivyo ni adui wa haki na jamii ielewe kuna maisha baada ya uchaguzi.
October 15, 2025
Home
Unlabelled
MBETO: TUTUNZE TUNU ALIZOTUACHIA BABA WA TAIFA
MBETO: TUTUNZE TUNU ALIZOTUACHIA BABA WA TAIFA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.



No comments:
Post a Comment