Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Mgombea nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendelea kuwawezesha watu wenye mahitaji maalum ili waweze kuendesha shughuli zao kwa tija zaidi.
Akizungumza katika mkutano na watu wenye mahitaji maalum katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil , Kikwajuni wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi. Dkt. Mwinyi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alisema atawawezesha zaidi awamu ijayo iwapo atachaguliwa tena kuwa Rais wa Zanzibar.
:"Natambua mambo mnayohitaji ni matatu katika uwezeshaji ikiwemo mafunzo ya ujasiria mali, kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia shughuli zenu na mikopo isiyo na riba" alisema.
Alibainisha kuwa mambo yote amesha anza kuyafanya na kwamba atayandeleza awamu ijayo kwa nguvu zaidi.
"Tutatoa mafunzo kwa ajili ya wote wanaofanya ujasiriamali ili shughuli zao wanazofanya ziwe na tija, tutaendelea kuweka mazingira bora ya kufanyia shughuli zao" alisema Dkt. Mwinyi.
Alisema mgombea huyo kuwa serikali yake itandelea kutoa mikopo kwa wenye mahitaji maalum kwa kadiri mikopo itakavyo imarika ndivyo fungu litakapokuwa kubwa zaidi.



No comments:
Post a Comment