HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

October 04, 2025

Mbeto: Upinzani Zanzibar wanachojua ni kupinga maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kimesema  upinzani wa   Zanzibar  unachojua ni  kupinga   maendeleo kwasababu tu yemeletwa  na   Serikali ya Mapinduzi (SMZ

Kutokana na hali hiyo, hata kama zitajengwa barabara za dhahabu Zanzibar ACT watapinga.

Pia CCM kimekumbusha katika vitabu vitakatifu kuwa hata Nabii Yusuf  alipingwa na makuhani  wa  Misri, aliposhika  madaraka akiwa Mtendaji Mkuu  wa dola  ya  kifalme huko Misri.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC ya CCM  Zanzibar, Khamis  Mbeto Khamis   aliyesema mantiki  ya kuwepo  upinzani  si kupinga na kubeza hata kwa mambo ya msingi. 

Mbeto  alisema anashangaa kuuona upinzani   hususan ACT Wazalendo, bila aibu  viongozi wake wamekuwa wakiipinga juhudi za  maendeleo  ya kisekta  yanayoonekana. 

"SMZ  chini  ya CCM, hata  ikijenga barabara za dhababu   , Majengo  ya shule   kwa kutumia  matofali ya  almasi na lulu,    ACT  kitabeza na kuita huo ni mkaa wa kuni za mikarafuu"   .

Mbeto alikitaja  kitendo cha upinzani kupinga kila jambo la maendeleo hakikuanzishwa na ACT kwani hata wahafidhina wa wakati huo, walipinga maendeleo yaliyokuwa yanaletwa na Afro Shirazi Party (ASP), chini ya Rais wa kwanza, hayati Abeid  Amani Karume pia  walimpinga  alipoleta maendeleo . 

"Maendeleo  hayakuwepo  Zanzibar enzi za ukoloni. Bila aibu  vibaraka na wapinga  maendeleo dhidi ya serikali ya ASP hawakuacha kubeza" alisema.

Mbeto alibainisha kuwa wapinzani  wa ASP  walidai SMZ  haijafanya lolote licha ya juhudi kubwa alizokuwa akifanya hayati Karume kuwaondoa waZanzibari katika umaskini.

Katibu huyo Mwenezi  alisema   hata  Nabii Yusuf  alipingwa na wapinzani  wake   asifanikishe sekta ya kilimo cha umwagiliaji na kujenga maghala   hivyo  ACT  kinapopinga  maendeleo ni  asili ile ile ya upinzani.

'Makuhani  wa Misri  walimbagua Nabii Yusuf  wakidai hana asili ya Misri. Wakamwita mshamba toka kijijini  Canaan huko  Palestina. 
Akafayiwa vituko  akwame kuleta maendeleo lakini alisimama imara akabadili Misri  kwa muda mfupi na ndio maana toka wakati huo hadi sasa Misri hakuna njaa" alisema.

Katibu  Mwenezi   huyo alisema kwa bahati nzuri wananchi wa Zanzibar  wameshapevuka kifikra na kupata mwamko wa maendeleo hivyo  wanajua kutofautisha ukweli  na  porojo za wanasiasa uchwara.

"Wananchi wameshuhudia  shule za ghorofa  zikijengwa, barabara, masoko, viwanja  vya ndege, bandari na madaraja yakijengwa. Wanajua   kutofautisha kati  ya  maendeleo na porojo za kisiasa za majukwaani" alieleza. 

Mbeto  alisema Mzee  
Karume  alipotekeleza  malengo ya   ASP na ya kimajumui hatimae    Tanganyika na Zanzibar zikaungana,  alichekwa na wapinzani wake. 

Katibu  huyo Mwenezi  alisema tabia ya kupinga kila kitu imekuwa   mila, desturi  na utamaduni kwa  upinzani wa  Zanzibar ambao pengine wangependa wananchi wabakie kwenye dimbwi la ufukara huku wakikosa huduma muhimu za elimu, afya na wakiwa hawana fursa zozote za kujikwamua kiuchumi.Upinzani Zanzibar wanachojua ni kupinga maendeleo

Mbeto: Hata nabii Yusuph alikataliwa Misri

Mbeto: Hata zikijengwa barabara za dhahabu ACT watapinga

Chama Cha Mapinduzi kimesema  upinzani wa   Zanzibar  unachojua ni  kupinga   maendeleo kwasababu tu yemeletwa  na   Serikali ya Mapinduzi (SMZ

Kutokana na hali hiyo, hata kama zitajengwa barabara za dhahabu Zanzibar ACT watapinga.

Pia CCM kimekumbusha katika vitabu vitakatifu kuwa hata Nabii Yusuf  alipingwa na makuhani  wa  Misri, aliposhika  madaraka akiwa Mtendaji Mkuu  wa dola  ya  kifalme huko Misri.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC ya CCM  Zanzibar, Khamis  Mbeto Khamis   aliyesema mantiki  ya kuwepo  upinzani  si kupinga na kubeza hata kwa mambo ya msingi. 

Mbeto  alisema anashangaa kuuona upinzani   hususan ACT Wazalendo, bila aibu  viongozi wake wamekuwa wakiipinga juhudi za  maendeleo  ya kisekta  yanayoonekana. 

"SMZ  chini  ya CCM, hata  ikijenga barabara za dhababu   , Majengo  ya shule   kwa kutumia  matofali ya  almasi na lulu,    ACT  kitabeza na kuita huo ni mkaa wa kuni za mikarafuu"   .

Mbeto alikitaja  kitendo cha upinzani kupinga kila jambo la maendeleo hakikuanzishwa na ACT kwani hata wahafidhina wa wakati huo, walipinga maendeleo yaliyokuwa yanaletwa na Afro Shirazi Party (ASP), chini ya Rais wa kwanza, hayati Abeid  Amani Karume pia  walimpinga  alipoleta maendeleo . 

"Maendeleo  hayakuwepo  Zanzibar enzi za ukoloni. Bila aibu  vibaraka na wapinga  maendeleo dhidi ya serikali ya ASP hawakuacha kubeza" alisema.

Mbeto alibainisha kuwa wapinzani  wa ASP  walidai SMZ  haijafanya lolote licha ya juhudi kubwa alizokuwa akifanya hayati Karume kuwaondoa waZanzibari katika umaskini.

Katibu huyo Mwenezi  alisema   hata  Nabii Yusuf  alipingwa na wapinzani  wake   asifanikishe sekta ya kilimo cha umwagiliaji na kujenga maghala   hivyo  ACT  kinapopinga  maendeleo ni  asili ile ile ya upinzani.

'Makuhani  wa Misri  walimbagua Nabii Yusuf  wakidai hana asili ya Misri. Wakamwita mshamba toka kijijini  Canaan huko  Palestina. 
Akafayiwa vituko  akwame kuleta maendeleo lakini alisimama imara akabadili Misri  kwa muda mfupi na ndio maana toka wakati huo hadi sasa Misri hakuna njaa" alisema.

Katibu  Mwenezi   huyo alisema kwa bahati nzuri wananchi wa Zanzibar  wameshapevuka kifikra na kupata mwamko wa maendeleo hivyo  wanajua kutofautisha ukweli  na  porojo za wanasiasa uchwara.

"Wananchi wameshuhudia  shule za ghorofa  zikijengwa, barabara, masoko, viwanja  vya ndege, bandari na madaraja yakijengwa. Wanajua   kutofautisha kati  ya  maendeleo na porojo za kisiasa za majukwaani" alieleza. 

Mbeto  alisema Mzee Karume  alipotekeleza  malengo ya   ASP na ya kimajumui hatimae    Tanganyika na Zanzibar zikaungana,  alichekwa na wapinzani wake. 

Katibu  huyo Mwenezi  alisema tabia ya kupinga kila kitu imekuwa   mila, desturi  na utamaduni kwa  upinzani wa  Zanzibar ambao pengine wangependa wananchi wabakie kwenye dimbwi la ufukara huku wakikosa huduma muhimu za elimu, afya na wakiwa hawana fursa zozote za kujikwamua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

Pages