NA DENIS MLOWE, MAFINGA
RAFIKI
Australia kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Cosato Chumi pamoja na Wizara ya Afya
(MOH), wamezindua mpango wa kuwagawia Taulo za kike wanafunzi wa shule
za Sekondari na Msingi katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Msaada
huo wa Taulo za Kike 500 umezinufaisha wasichana wa Shule ya Sekondari
Kinyanambo na Shule ya Msingi Mkombwe zilizoko Mafinga.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo, Afisa mradi , Saum Zidadu alisema kuwa
hatua ya Rafiki kuanzisha kampeni ya Rafiki wa Binti ni sehemu ya kuunga
mkono jitihada za kumpatia mtoto wa kike hedhi salama.
Alisema
kuwa wanataka kuhakikisha msichana wa Kitanzania anabaki shuleni,
anaendelea kusoma na kufikia ndoto zake bila kuzuiliwa na hedhi,.
Alisema
tofauti na taulo za kibiashara zinazotumika mara moja na kutupwa, taulo
hizi za kisasa zinazoletwa na Rafiki zinaweza kuoshwa na kutumika tena
hiyo yote ni katika kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Wizara ya
Afya, na kwa hamasa ya Cosato Chumi,.
Aliongeza
kuwa Rafiki imeanzisha Rafiki wa Binti kwa lengo la kuwasaidia
wasichana wa Kitanzania kupata huduma hii ya taulo za afya kwa nia ya
kulinda afya zao, kuokoa muda ambao unapotea na hivyo kuwezesha kufikia
malengo yao.
Ifahamike kuwa Wizara ya Afya
ilizindua Mwongozo wa Kitaifa wa Afya na Usafi wa Hedhi wa mwaka 2025
ili kuwawezesha wasichana kusimamia hedhi zao kwa heshima. Mwongozo huu
unaonyesha kuwa wasichana wengi nchini Tanzania hukosa hadi 25% ya siku
za masomo kwa sababu ya kushindwa kudhibiti hedhi zao. Wengi wao pia
wanakosa maarifa sahihi kuhusu afya na usafi wa hedhi.
"Rafiki
wa Binti imejitolea kusaidia Halmashauri ya Mafinga. Hii inaanza leo
kwa kugawa ‘Binti Packs’ 500, kila moja ikiwa na taulo sita za kike
zinazoweza kutumika tena, kitabu cha elimu, na begi la kuhifadhia"
Alisema
Alisema kuwa Msaada huo umetolewa bure
kabisa kwa wasichana wa shule, pamoja na elimu ya kubalehe na hedhi,
vipimo sahihi vya taulo za kike ,maelekezo ya usafi, matumizi na namna
ya kuosha.
Taulo za kike zimekuwa zikitumika
kibiashara kwa zaidi ya muongo mmoja. Inakadiriwa kuwa duniani kote,
zaidi ya milioni 15 za taulo hizi huuzwa kila mwaka. Huko Australia,
takribani robo ya wasichana wanatumia taulo za kike za na umaarufu wake
unaongezeka haraka.
Taulo hizi ni za
kiubunifu kwa uwezo mkubwa wa kufyonza, salama kutumia na rafiki wa
mazingira. Zikitunzwa vizuri, zinaweza kutumika tena kwa miaka miwili.
Rafiki
wa Binti itaingia kwenye ushirikiano na wadau na shule ili kurahisisha
ugawaji wa Binti Packs pamoja na elimu ya hedhi. Rafiki imejikita katika
kuhakikisha msaada huu ni endelevu na kufanikisha upanuzi wa mradi huu
ndani ya Halmashauri ya Mji Mafinga na maeneo mengine ya Tanzania.





No comments:
Post a Comment