HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 22, 2025

Utafiti Kura ya Maoni wambeba Samia Uchaguzi Mkuu

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, anaongoza kwenye kura za maoni kwa asilimia 84.5 dhidi ya wagombea wenzake anaochuana nao katika nafasi hiyo ya juu kabisa kwenye muundo wa Serikali, uchaguzi Mkuu ukitarajiwa kufanyika siku chache zijazo, Oktoba 29, 2025.

Takwimu hizo ni kulingana na utafiti wa kura za maoni uliofanywa na Kituo cha  Sera za Kimataifa kwa Ukanda wa Afrika (Centre for International Policy- Africa (CIP- Africa) ambapo Mkurugenzi wa Tafiti na Uchapishaji wa Kituo hicho, Thabit Mlangi amesema mgombea anayefuata katika kura hizo za maoni ni Salum Mwalimu, Mgombea wa Urais kupitia CHAUMMA akiwa na asilimia tatu za kura za maoni.

Kulingana na Kituo hicho cha CIP- Africa, jumla ya wananchi 1976 walihojiwa katika kura hiyo ya maoni, asilimia 100 wakiwa si tu wana sifa za kushiriki uchaguzi Mkuu bali pia wamejiandikisha katika daftari la Mpigakura na wanavyo vitambulisho vya mpigakura katika uchaguzi mkuu ujao.

CIP- Africa katika kutekeleza majukumu yake imekuwa ikishiriki katika michakato mbalimbali ya uchaguzi barani Afrika kupitia tafiti, kura za maoni, uangalizi wa uchaguzi, midahalo na mikutano ikishirikiana kwa karibu na  na Institute of Security Studies (ISS) ya Afrika Kusini, Electoral Institute for sustainable Democracy in Africa (EISA) yenye Makao makuu yake Geneva Uswis na yenye Makao yake ya Kanda Nairobi nchini Kenya pamoja na Africa Think- tank Dialogue iliyopo Cape Town, Afrika Kusini.

Amesisitiza kuwa utafiti huo ulifanyika katika mikoa 17 ikiwemo Dar es Salaam, Tabora, Kagera, Dodoma, Tanga, Mbeya, Ruvuma, Morogoro, Geita, Arusha na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages