NA DENIS MLOWE, IRINGA
FADHILI
Ngajilo mgombea ubunge Iringa mjini kwa tiketi ya CCM amesema kwamba
endapo akichaguliwa atalivalia njuga suala la wafanyabiashara ya
Kitanzini - Miyomboni kufanya biashara masaa 24 kutokana kata hiyo kuwa
ya wafanyabiashara wengi.
Ngajilo alisema
kwamba jimbo la Iringa mjini linaongozwa na wafanyabiashara ambao
asilimia kubwa wako katika kata ya Kitanzini Miyomboni ambapo kuna soko
kuu la Iringa, soko la Magari mabovu na kila aina ya biashara halalli
inafanyika hapo hivyo kuna umuhimu wa kuanzisha biashara masaa 24.
Alisema
ili kufanikisha hilo watakaa chini kama halmashauri na kuketi na
jeshipolisi kulinda usalama wa wafanyabiashara na kufungwa mataa kwa
ajili ya usalama kwa maeneo ya kata hizo.
Alisema
kuwa nchi nyingi duniani wanafanya biashara usiku na aliyesema watu
walale usiku ni nani alihoji Ngajilo na kuongeza kuwa lengo ni kuinua
kipato cha mwananchi wa jimbo la Iringa.
Alisema
endapo atapewa ridhaa hiyo na wananchi wataichagua serikali iongozwe na
CCM watahakikisha wanajjenga Machinga Complex ambalo wafanyabiashara
watafanyia biashara kwa utulivu.
Aidha
aliongeza kuwa watahakikisha kwa kushirikiana na diwani wa Miyomboni
Kitanzini watarekebisha soko la Kitanzani liwe la kisasa kuliko lilivyo
sasa.
Ngajilo akizungumzia kuhusu Suala la
makazi katika kata hiyo atahakikisha yanarasimishwa kwa wale ambao bado
na kuhakikisha wanapata vibali vya kukarabati makazi kwa wakati.
Suala
la afya alisema kuwa wataendelea kuongeza idadi ya vituo vya afya
ambavyo viko katika ilani ya CCM na kuwataka wananchi wawape kura za
kishindo katika mafiga matatu kwa maana ya Rais Samia , wabunge na
madiwani.






No comments:
Post a Comment