HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 06, 2025

CCM: Demokrasia ipo katika sanduku la kura

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM),  kimesema siku ikitokea kikashindwa Uchaguzi Mkuu  kwa matakwa ya kura za wananchi hakitasita kukubali matokeo   lakini sio kugawa madaraka kama hisani kwa chama chochote cha siasa.

Akizungumza, Mjini Unguja, 06 Oktoba 2025 kufuatia hoja ya ACT Wazalendo ya kutaka kugawana madaraka, Katibu  wa Kamati Maalum ya NEC  za Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi  na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis alisema madaraka hayatolewi kwa hisani, huruma wala ushemeji isipokuwa ni chama kukubalika kwa umma.


Mbeto alisema CCM  kimesistiza  upinzani wa Zanzibar   haujapevuka na kuwa madhubuti kiasi cha kuwaridhisha wananchi ushike madaraka.

Chama hicho Mbeto alisema, mgombea wa nafasi ya Rais Zanzibar kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman atambue kuwa bado  watu hawakijakiamini chama chao kwa itikadi na kukosa sera nae kubaki na misimamo yake na aina ya viongozi  walionao  ili kipigiwe kura za kushika utawala.

Alisema  Wananchi  hususan wa Zanzibar ni wakomavu kisiasa, werevu wanaopima mambo bila kukurupuka hivyo hawajapata sababu  ya kukiacha CCM na kuuchagua upinzani.

'Upinzani bado   una kazi ya kujitafakari. Lazima  wajue kwanini wananchi wanawakataa, matamshi  yao hayaonyeshi kujali umoja, wananadi ubaguzi mambo ambayo hayakubaliki popote" alisema Mbeto 

Katibu Mwenezi huyo alisema kujenga taasisi ya kisiasa imara inayoaminiwa na wananchi, si jambo  la muda mfupi, badala yake ni mchakato unaohitaji kupata  sera mbadala , hoja  yakinifu na dira sahihi.

"ASP toka mwaka 1957 kimevibwaga vyama vya  ZNP na ZPPP na ilitokea hivyo havikutokana na matakwa ya wengi. Wananchi wote waliunga mkono sera za ASP na wagombea wake" alibainisha na kuongeza kuwa ACT inatakiwa ijifunze kupitia historia.

Mbeto alisema kizazi cha sasa kuelekea miaka hamsini ijayo,ni kile kilichotokana na Mapinduzi  
ya Zanzibar  mwaka 1964 ambayo ndiyo yaliovunja matabaka  na utawala uliodumu  miaka takribani 104 iliyopita.

"Makundi ya wananachi wa kizazi hiki  wamesomeshwa kwa chini ya sera za CCM ambazo zimerithiwa toka TANU na ASP chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambazo zimekomesha ubaguzi,  upendeleo na kuwajali wanyonge na masikini " alisema. 

Alisema  wanapotokea wanasiasa wa upinzani kuanza kuhubiri sera zisizoijengea matumaini kwa jamii wana haki ya kuvikataa vyama hivyo . 

"Mgombea anaposema utatoa nchi  taka usitake huyo ameshabaini  atashindwa ndio maana anatumia lugha ya vitisho" alisema Mbeto.


No comments:

Post a Comment

Pages