HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 04, 2026

Yanga SC yaanza kwa kishindo NMB Mapinduzi Cup 2026, yaifumua KVZ

MABINGWA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga, wameanza kwa kishindo Mashindano ya NMB Mapinduzi Cup 2026, baada ya kukichakaza Kikosi cha Volunteers Zanzibar 'KVZ' kwa mabao 3-0.

‎Ushindi huo wa kikosi cha Yanga chini ya Mreno Pedro Goncalves, ndio mkubwa zaidi tangu kuanza kwa michuano hiyo inayodhaminiwa na Benki ya NMB , iliyoanza kutimiza vumbi Desemba 28, 2025 kwenye dimba la New Amaan Complex Zanzibar. 


‎Mabao ya Yanga katika mechi hiyo iliyochezwa jioni hii yamefungwa na viungo wake Pacome Zouzoua, Celestine Ecua na nyota mpya Mitaa ya Twiga na Jangwani, Emmanuel Mwanengo. 

‎Katika mchezo huo, kiungo wa Yanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Maxi Nzengeli aliibuka na Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi na kuzoa kiasi cha Sh. mil. 1 inayotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

‎Aidha, Majid Khamis wa KVZ aliibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Mwenye Nidhamu Zaidi 'NMB Most Discipline Player ' inayotolewa na Mdhamini Mkuu wa Mashindano hayo NMB, ikiambatana na kitita cha Sh. 500,000.


Yanga watarejea tena dimbani Amaan Complex, Jumanne Januari 6 kuwavaa Wakusanya Kodi wa TRA United (zamani Tabora United). Yanga watahitaji ushindi ama sare dhidi ya TRA ili kufuzu nusu fainali ya mashindano, ambayo Bingwa hujinyakulia Sh. Mil. 150 na mshindi wa pili kuvuna Sh. Mil. 100.

No comments:

Post a Comment

Pages