HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 10, 2026

MCHANGO WA SEKTA YA MAFUTA NA GESI ASILIA NI MKUBWA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA

 NA HELLEN NGOROMERA


USIMAMIZI na udhibiti madhubuti wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali hizo zinatumika  kwa manufaa ya Watanzania.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti mkondo wake Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni amesema hayo leo Julai 10 katika. Kongamano la Siku ya Nishati  lililofanyika katika Ukumbi wa Mwandoro ndani ya Viwanja vya Sabasaba kunakofanyika Maonyesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.



"Ni muhimu kuwa waangalifu katika usimamizi na udhibiti katika shughuli za PURA kwani hali hiyo italeta manufaa kwa wananchi na nchi kwa ujumla," amesema Sangweni.


Ameongeza kuwa sekta ya mafuta na gesi asilia ina mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa kupitia uwekezaji, ajira na mapato ya serikali.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo mkuu kuna umuhimu wa kuendelea kuvutia uwekezaji kwenye sekta hiyo pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na wadau ili.kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika mafuta na gesi asilia.


Kongamano hilo limewakutanisha viongozi, wadau mbalimbali wa nishati, wawekezaji na  washirika wa maendeleo ili kujadili masuala mbalimbali ukiwemo  mwelekeo wa sekta ya nishati na fursa za uwekezaji.



No comments:

Post a Comment

Pages