HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

August 12, 2026

NANE NANE YATAKIWA KUTUMIKA KWA AJILI YA UWEKEZAJI WENYE TIJA


Maafisa wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS wakitoa elimu kwa wadau waliotembelea banda la kampuni hiyo wakati wa Maonesho ya Nane Nane jijini Dodoma.


NA MWANDISHI WETU


KATIKA dunia ya leo ambayo kila sekunde kuna hitaji jipya la kifedha mlangoni mwako bila ya kujali hali ulinayo, ni muhimu kufikiria namna bora ya kufanya uwekezaji wenye tija utakaowezesha kufikia malengo ya kifedha.


Ikiwa tunaadhimisha siku ya Nane Nane, wanaweza kutumia Mifuko ya Uwekezaji ya UTT AMIS kufikia malengo yao ya kifedha.


Unafahamu sehemu mbalimbali za uwekezaji kama ufugaji, kilimo na biashara.

Hata hivyo, kuna sehemu nyingine mbadala za uwekezaji tunazoweza kuwekeza fedha na hatimaye kufikia malengo yako.


Moja ya sehemu hizo ni kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja chini ya uongozi na ushauri wa karibu wa msimamizi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja nchini, UTT AMIS.

Ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika Masoko ya Mitaji , UTT AMIS imekuwa daraja la kuwezesha wananchi kiuchumi kwa kuleta ushiriki mpana wa uwekezaji kwenye Masoko ya fedha na Mitaji kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja.


Ikiongozwa na sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya mwaka 1994 pamoja na marekebisho yake na kanuni ndogo za uwekezaji wa mifuko ya pamoja ya 1997, UTT AMIS inasimamia mifuko sita ya uwekezaji ambayo ni; Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Kujikimu, Ukwasi na Hatifungani. mbali na usimamizi mifuko hiyo, taasisi hiyo imekuwa ikitoa huduma ya usimamizi wa fedha binafsi.


Akizungumza ofisini kwake, Mkuu wa Mawasiliano  na Uhusiano wa UTT AMIS, Rahim Mwanga amesema wigo wa utoaji huduma za uwekezaji wa pamoja umezingatia makundi yote; yaani kuanzia watoto, watu wazima, watu binafsi, wafanyabiashara, vikundi, mashirika na kampuni.


Utaratibu wa uendeshaji

baada ya kupata kibali kutoka kwa CMSA, UTT AMIS huandaa waraka wa matarajio wa namna ya mfuko utakavyoendeshwa na kisha kibali cha kuanzisha mfuko hutoka, ameeleza Mkurugenzi.


Hatua inayofuata baada ya mfuko kuanzishwa ni ukusanyaji wa rasilimali fedha kutoka kwa wawekezaji mbalimbali na kuziwekeza katika masoko ya mitaji na fedha kwa niaba yao na baada ya kupata faida huzirejesha kwa wawekezaji kwa uwiano sawa na kiwango kilichowekezwa.


“Sehemu ya uwekezaji wako kwenye mfuko inaitwa kipande,” amesema.

Amesema hilo linafanyika kwa lengo la kutengeneza wigo mpana kwa wawekezaji wote, hususan wadogo kupata urahisi wa kushiriki katika masoko ya mitaji.

Amedokeza kima cha chini cha uwekezaji kinaanzia Sh5000 na kuendelea kulingana masharti ya mfuko husika.

 

Faida za uwekezaji

“Mwekezaji anafaidi mseto wa wawekezaji. Mseto hufanyika ili kuhakikisha usalama wa fedha za mwekezaji, faida shindani na ukwasi kwa wawekezaji,” ameeleza Mkuu huyo, akitaja mseto kama faida ya kwanza katika uwekezaji wa pamoja.


Faida nyingine, ni ukwasi, yaani urahisi wa mwekezaji kupata fedha zake baada ya kuwekeza, ambapo huchukua muda wa siku tatu hadi kumi za kazi kulingana na masharti ya mfuko husika.


“Jambo lingine zuri kuhusu mifuko hii ni kwamba uwekezeji hufanyika kwa weledi mkubwa ikijumuisha ushauri kutoka kwa maofisa wa UTT AMIS wenye ufahamu na uzoefu wa soko ili kuwezesha mwekezaji kufikia malengo yako,” amefafanua zaidi.


Jambo lingine zuri zaidi ni kwamba mifuko hiyo iko chini ya uangalizi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), ameeleza zaidi.


Uwekezaji wenye tija

UTT AMIS haihamasishi kuwekeza tu, bali wawekezaji wafanye uwekezaji  wenye malengo ili kupata tija. Amesema ili uwekezaji wenye tija utokee, ni lazima kuwe na lengo lililowazi mfano kujianda na kustaafu, ada za watoto, kisha muda wa ufikiaji lengo unaweza kuwa mwaka 1,3,5 au zaidi, mkakati wa kuwekeza (inaweza kuwa kila siku, wiki au kwa mwezi) kulingana na hali ya kifedha ya muhusika, kiasi cha faida inayotarajiwa na uwezo wa kubeba hatari za uwekezaji.


Mfano; Ukiwa na hitaji la Sh. milioni 10 ili kununua kiwanja ndani ya miaka 3 na faida tarajiwa ya ukuaji kila mwaka ya asilimia 12 ya uwekezaji ni muhimu kufanya tathmini kujua unatakiwa kuwekeza kiasi gani kila mwezi ili uweze kufikia lengo na kama unaweza  kumudu kiasi hicho.


Ukweli ni kwamba, baada ya mahesabu, utatakiwa kuchangia 232,144/- kwa kila mwezi, atakuwa amewekeza  8,357,151.53/- faida tarajiwa ya 1,642,848.47/-  baada ya miaka mitatu.

Hivyo kukamilisha lengo lake la shilingi 10,000,000/-

Mwanga amefafanua kuwa faida ya mfuko hutegemeana na hali ya soko, hivyo wakati mwingine hupanda na kushuka.


Faida na ukuaji wa rasilimali za mifuko

Kulingana na Mwanga mifuko hiyo imeendelea kukua kwa kasi kwani mpaka kufikia Machi 2026, jumla ya mali za mifuko yote ni zaidi ya shilingi trilioni 4.6 

Mfuko wa Umoja ukipata faida ya asilimia 34.6, Wekeza Maisha (20.35), Watoto (20.64), Kujikimu (21.8), Ukwasi (12.6) na Hatifungani (12.1). Amesema pia wawekezaji wote waliosajiliwa wanafikia zaidi ya 600,000  

Ukuaji huo kwa kiasi kikubwa amesema unachangiwa na imani ya wawekezaji, hali ya utulivu wa soko na ukwasi wa kutosha sokoni.

 

Huduma

Katika eneo la huduma, UTT AMIS imekuwa ikitanua wigo wa ufikishaji huduma za uwekezaji kila kona kupitia mtandao wake wa matawi nchini. Kampuni hiyo inayo ofisi zake katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya , Zanzibar, Morogoro na Shinyanga-Kahama


“Pia tuna kituo cha huduma kwa wawekezaji,unapiga namba ya bure 0800112020 kwa ajili ya kupata maelezo zaidi kuhusu huduma zetu,” amesema Mwanga.


Sambamba na hilo UTT AMIS imehakikisha huduma za uwekezaji zinasogea kwa kila Mtanzania kupitia  huduma ya “UTT AMIS App na UTT AMIS Investor Portal. Kupitia huduma hizo mtu anaweza kufungua akaunti ya uwekezaji, kuanza kuwekeza, kutoa fedha zake alizowekeza kwa hadi kiasi cha shilingi milioni 5 kwa siku na kupata taarifa zake za uwekezaji.


“Tumekwenda mbali zaidi kwa kuhakikisha pia wawekezaji wanaweza kununua vipande kupitia njia zote za mitandao ya simu na benki zote popote walipo ,” amedadavua.

Mwanga amesema kuwa huduma za Mifuko ya UTTAMIS hizo pia zinapatikana kupitia ofisi za Madalali wote wa Soko la Hisa la Dar es Salaam na kwa wakala ambaye ni katika kila tawi la Benki ya CRDB hapa nchini.


Hitimisho

Ili kufikia malengo yako kwa urahisi, kama mwekezaji, ni muhimu kuanza kuwekeza mapema na mara kwa mara. Mifuko bado inakupa uhuru wa kuwekeza wakati wote ili kufikia malengo hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages