HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 25, 2015

HATIMAYE KINYESI CHA MWALIMU CHATEKETEZWA


Mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke Kitengo cha Usafishaji, Ramadhani Athuman akiweka dawa katika vyombo alivyokuwa akitumia kuhifadhia kinyesi mwalimu Gaudensia Albert wa Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam, kabla vyombo hivyo havijaenda kutupwa dampo. (Picha na Francis Dande)

 Umati wa watu ukiwa nje ya nyumba wakati zoezi la kuteketeza kinyesi likiendelea.
 Mlango ukivunjwa ili maofisa wa afya waweze kuingia ndani ya chumba cha mwalimu.
 Kinyesi kikiwa kimehifadhiwa ndani ya chumba cha mwalimu.
 Wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke wakiondoa kinyesi katika nyumba ya mwalimu Gaudensia.
 Wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke wakiondoa kinyesi katika nyumba ya mwalimu Gaudensia.
Maulid Liuguyo ambaye ni mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke kitengo cha usafi akishiriki katika zoezi hilo. 

Na Mwandishi Wetu

Manispaa ya Temeke leo imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo.

Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Yombo, Kisiwani Kata ya Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na wakishirikiana na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo walilipata juzi juzi jioni, baada ya kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa Kata hiyo wafanye utafiti wakujua tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani.

“Baada ya kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika, ambapo tulischukua jukumu la kwenda kumhoji Mkuu wa washule hiyo ili kujua kama mwalimu Gaudensia alikuwa na akili timamu au la, hata hivyo, Mkuu wa shule atueleza kuwa alikuwa na akili timamu,”alisema Tembo.  

Alisema pamoja na kuutekeza mlundikano huo wa kinyesi pamoja mikojo na matapishi bado wanaendelea na utaratibu wa kumfikisha mwalimu huyo kwenye vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka.

“Hili tukio halihusiani na ugonjwa wa akili inawezekana kuna tatizo lingine ingawa hatuwezi kuamini mambo ya ushirikina lakini haiwezekani mwalimu kama yule ajisaidie na kuhifadhi uchafu kama ule ndani,”alisema.

Aidha, alisema mwalimu huyo hakuweza kufika kwenye eneo la tukio hali iliyofanya mlango wa chumba chake uvunjwe chini ya uwaangalizi wa polisi.

Tembo, alisema mwalimu huyo alishindwa kutokea kwenye eneo la tukio kwa vile alipelekwa Hospitali ya Temeke kisha kuhamishiwa Haspitali ya Taifa muhimbili kwa ajili ya kupimwa afaya baada ya kupata mshituko ambao umesababishwa na taarifa hizo.

Afisa Afya wa Usafi wa Mazingira, Jumamne Muhogo, alisema uchafu walioubaini ulikuwa ni uchafu wa kinyesi, mikojo na matapishi inasemekana kuna kipindi alikuwa anatapika.

Pia alisema kipo kifungu cha sheria, walifika pale maofisa kutoka idara mbalimbali kupima uzito wa tukio, ambapo kama wangemkuta wangemkamata kwa hatua za kimfikisha mahakamani.
Mhogo, alisema hata kama alikuwa mtaalamu wa sayansi, alikuwa amehifadhi uchafu ule kwa ajili ya utafiti basi hayo yote angekwenda kuyaeleza mahakamani. 

“Tukio hili kwa manispa ya Temeke ni la kwanza kutokea yani inaekekea huyu mtu hana akili ya kawaida kama angekuwa na akili za kawaida asingeweza kufanya na mna hii,”alisema.


Umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo walikusanyika kwa wingi tangu saa tatu asubuhi wakisubiri kazi hiyo hadi ilipofnyika saa tisa jioni na wataalamu wa manispaa hiyo.

Wataalamu hao walimwagia dawa uchafu huo kisha kuanza ubeba na kutumbukiza chooni kwa uangalifu mkubwa.
Walipomaliza walvisafisha vyombo hivyo kwa kutumia dawa ambazo zimeweza kusaidia kuondoa harufu mbaya iliyokuwa imezagaa hewani.

Awali, Sajenti wa Jeshi la Polisi  Ramadhan Kagolo, alisema aliwajibika kusimamia kuvujnjwa kufuli la chumba hicho kwa vile kazi iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda afya ya jamii.

Tukio hilo ambalo limekuwa likifuatiliwa na majirani hususan jana wakati wa uteketezaji lilitokea Februari 22 mwaka huu.  

2 comments:

  1. Ni taarifa za kashtua, ajabu, na inaniacha na maswali mengi yasiyo na majibu. Hebu mwandishi naomba fuatilia hizi habari kwa mhusika utupe details kwani nashindwa kuamini kama ni kweli au maigizo. Jitume usichoke kutulisha hii habari ya maajabu makubwa sana.

    ReplyDelete

Pages