HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2019

PAMBANO LA CRDB NA WABUNGE KATIKA PICHA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela na kapteni wa timu ya mpira wa miguu ya Benki ya CRDB akimtambulisha kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa mchezaji wa timu Abdul Van Mohammed wakati timu hiyo ilipocheza na timu ya Bunge FC . Timu ya mpira wa miguu ya Benki ya CRDB iliifunga timu ya Bunge FC kwa mikwaju ya penati 3 kwa 1 katika Bonanza lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akionyesha Kombe la Ushindi baada ya kukabidhiwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa (wa pili kushoto). Timu ya mpira wa miguu ya Benki ya CRDB iliifunga timu ya Bunge FC kwa mikwaju ya penati 3 kwa 1 katika Bonanza lililofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakishangilia ushindi baada ya kuifunga timu ya Bunge FC kwa mikwaju ya penati 3 kwa 1 katika Bonanza lililofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Pages