Waziri
wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (kushoto), akimkabidhi kombe, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma
Shirikishi Benki ya CRDB, Esther Kitoka, baada ya benki hiyo kushika nafasi
ya pili, katika hafla ya utopaji tuzo za Mwajiri Bora Tanzania 2012
zilizofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa na tuzo tatu walizoshinda katika hafla ya utoaji wa tuzo za Mwajiri Bora.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi Benki ya CRDB, Esther Kitoka
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi Benki ya CRDB, Esther Kitoka
DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya CRDB imejishindia tuzo tatu
ikiwamo ya Fedha kwa kushika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha Tuzo za
Mwajiri Bora wa Mwaka 2012, zilizohusisha zaidi ya Kampuni 30, ambayo ilipokelewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa benki
hiyo Esther Kitoka.
Hafla ya kukabidhi tuzo hizo zilizoandaliwa na
Chama cha Waajiri nchini Tanzania (ATE) , ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Akiongea wakati wa kukabidhi tuzo hizo, Rais
Kikwete, aliwashukuru waajiri Wakitanzania, mashirika ya umma na binafsi kwa
kazi nzuri waliyoifanya katika kuisadia Serikali kutengeneza ajira na maendeleo
ya uchumi na pia alikiri uwepo wa tatizo la ajira hapa nchini.
“Ninayo furaha kushiriki nanyi jioni ya leo.
Mmekuwa msaada mkubwa kwa taifa letu na ninapenda kuwaahidi kuwa Serikali
itawasaidia katika shughuli zenu,” alisema Rais Kikwete.
Aidha Rais Kikwete aliongeza kuwa, juhudi za
Serikali pekee haziwezi kuifanya nchi ya Tanzania kuwa yenye kipato cha kati
labda kama kutakuwa na juhudi kati ya Serikali na sekta binafsi ambazo
zitasaidia kupunguza idadi ya Watanzania
wasio na ajira nchini.
Rais Kikwete ametoa changamoto kwa Chama cha
Waajiri Tanzania (ATE) na Serikali kufanya kazi kwa pamoja katika masuala
mawili muhimu ambayo ni maendeleo ya rasilimali watu hasa katika uendelezaji wa
ushirikiano wa maendeleo kati ya taasisi za vyuo vya juu na viwanda.
No comments:
Post a Comment