KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Tanzania, Muashamu Kadinali Polycarp Pengo (pichani juu), amewaonya baadhi ya wanasiasa na taasisi kuacha kuwashinikiza
wananchi kutoa maoni ya mchakato Katiba Mpya kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Kadinali
Pengo aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari jijini
Dar es Salaam leo, kuhusu ujumbe uliotolewa na maaskofu kwenye mkutano wa
viongozi hao, uliyofanyika Oktoba 7 hadi 28 mwaka huu, huko Rome, Italia.
Alisema kwa kuwa Katiba linagusa maslahi ya nchi
hivyo ni vyema kila mwananchi akatumia fursa yake ya kuwasilisha maoni yake
mwenyewe.
“Watu waruhusiwe kutoa maoni yao, lakini lazima
tukubaliane kuwa kila mtu ana maoni yake na maoni yote hayewezi kuingizwa
katika katiba hiyo,” alisema.
Alisema kuna mfumo ambao baadhi ya nchi umetumia
kwa kuandaa katiba mbili kisha kutafutwa watu maalumu wakukabidhiwa katiba hizo
kisha wakaandaa katiba mpya.
Katika hatua nyingine Kanisa hilo limewataka
viongozi wenye dhamana kuacha kushabikia udini katika kusimamia haki za jamii
ya Kitanzania.
Askofu Pengo alisema wapo watu makini wenye uwezo
wa kusimamia mchakato huo ikiwemo Tume iliyoteuliwa kusimamia mchakato huo.
Alisema nchi hii imegawanyika katika madhehebu
mbalimbali hivyo, inapotokea dhehebu moja
kulitukana na kuharibu mali za lingine, serikali haipaswi kukaa kimya
bali inachotakiwa ni kusimamia haki za makundi yote na si kubagua.
“Suala Sheikh
Ponda sijalifuatilia lakini kama kweli hayo yaliyotokea kwa kuchomwa
makanisa, lazima serikali ishughulikie uharibifu wa mali hizo za dini na
madhehebu yote haipaswi kubagua”alisema
Askofu Pengo alisema endapo serikali itaamua
kulishughulikia suala hilo kwa upande mmoja na kuacha maswali kwa wengine basi
itakuwa imekwenda kombo.
Alibainisha kuwa malalamiko yanapotolewa na mtu
kama yeye huwa hayana nguvu sana katika jamii kuliko yanapotolewa na Rais wan
chi.
Askofu Pengo alisema Rais ana ngucu kubwa kwamba
kila analolisema huwa linapokelewa kwa uangalifu mkubwa katika.
“Ni lazima viongozi wajiepushe katika kupenda ubaguzi
wa kdini kwa mfano Mkapa hakuweza kusema wakatoliki wenzangu na nyiye wenye
mapenzi mema kwa lengo la kutekeleza majukumu ya maendeleo”alisema.
Askofu Pengo alitoa tahadhari kuwa Rais siyo lazima
awe Mkatoliki au muislam, bali anapochaguliwa anakuwa Rais wa nchi hii
ilikuwatumikia watu wote ambapo pia
anapaswa kulinda, kusimamia na kulinda mali za madhehebu yote na si vinginevyo.
Akizungumzia kuhusu ujumbe wa heri ya Chrismas na
mwaka mpya, ambao ni kutoka kwenye mkutano huo, wa Rome na kuelekezwa katika
Bara la Afrika, Askofu Pengo alisema maskofu wa Sinod, wamewapongeza waumini
wao kwa kudumisha imani.
Alitanabaisha kuwa licha ya mazingira magumu
ikiwemo uchumi duni, njaa maradhi na imani potofu za kidini, bado wameweza kustahimili na kuwafanya kubaki kitu
kimoja.
Vilevile alisema Kanisa limeweza kuwaleta kaleta
waamini karibu na kuwa familia ya mungu ambapo kwa Afrika neno familia lina
maana kubwa kwani hujenga udugu na ujamaa katika jamii.
Askofu Pengo alibainisha kuwa familia ya mungu
haibaki katika dhehebu fulani, bali neno hilo linasaidia kuwa watu wote wenye
mapenzi mema kuwa wa familia moja.
“Kutofautiana katika jamii ni jambo la kawaida na
kisha watu hurudi na kubaki familia moja”alisema
Aidha, kuhusu mihadhara ya kidini, Askofu Pengo alisema hakuna mtu mwenye haki ya
kumtukana mtu kutokana na imani yake.
Alisema kama serikali inashindwa kuwakemea wanaowatukana wengine anaogopa, hali ikiachwa iendelee hivyo ianaweza kuvuruga amani
na mshikamano na nchi kuingia kwenye mgogoro.
Alisema haoni tatizo kama mtu atasema Yesu si mwana
wa Mungu katika nia ya mtazamo wake hapo kutakuwa hakuna tatizo kwa kuwa hata
yeye anaweza kusema Mohamed siyo Mtume tena kwa ushahidi kutokana wa vitabu vya
dini alivyosoma.
Kuhusu elimu nchini, Askofu Pengo alisema watu wote wenye nia njema na
mapenzi ya nchi hii wanapaswa kutoa kipaumbele ili kila Mtanzania apate elimu
iliyo bora.
Alisema hapendezwi na mpango wa elimu inayotolewa nchini kwani mfumo wa
baadhi ya shule nyingi zimekuwa kitega uchumi hivyo kuwa kikwazo kwa watu
wenyekipato cha chini.
Askofu Pengo alisema hali hiyo ikiachiwa iendelee
inaweza kuja kuwafanya wale waliokosa elimu kuvuruga amani kwa kudaai haki zao
za kioungozi na maslahi mengine.
No comments:
Post a Comment