TANZANIA
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Vijana wa Kanda ya Afrika
wa Jumuiya ya Madola kuanzia Januari 28 hadi Februari Mosi, mwakani.
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika ya Mpango wa Vijana
wa Jumuia ya Madola, James Odit, aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati alipokuwa kizungumza
na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara
kuhusu maandalizi ya mkutano huo.
Mkurugenzi huyo, alisema mkutano huo utahusisha nchi 22 ambazo ni wanachama na jumla ya washiriki 60
wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo kutoka katika wizara zinazohusiana na
masuala ya vijana, viogozi wa vijana, viongozi wawakilishi wa Baraza la Vijana,
wawakilishi wa kimataifa, viongozi wa kikanda wa maendeleo ya vijana na Jumuiya
ya Madola.
Miongoni mwa mambo mengine
waliyojadiliana ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Vijana na jinsi ya kuunda
Katiba ya Baraza la Vijana la Jumuiya ya Madola.
“Mkutano huu utajadili namna ya kuunda
Baraza la Vijana la Jumuiya ya Madola (CYC), program za maendeleo ya vijana na
jinsi ya kuwawezesha katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo,” alisema Odit.
Kwa Upande wake Waziri wa wizara
hiyo, Dk. Mukangara alisema anaishukuru jumuiya hiyo kwa kuichagua
Tanzania kuwa mwejeji wa mkutano huo.
Hata hivyo, aliema suala la uundaji wa Baraza la Taifa la Vijana
hivi sasa liko katika hatua ya ngazi za juu.
Dk. Mukangara alizitaja baadhi ya
changamoto za kuendeleza mipago mbalimbali ya maendedeleo ya vijana kuwa ni
pamoja na ukosefu wa fedha za kutosha, mfano kama vile kuwawezesha
vijana katika shughuli za kiuchumi na kimaendeleo, kuwajengea uwezo, kuwapatia ajira, ujuzi na elimu.
Waziri
Mukangara aliishauri Jumuiya hiyo kuangalia namna ya kushirikiana
katika maeneo mengine kama vile sekta ya Michezo, Utamaduni na Habari.
Does your website have a contact page? I'm having problems locating it but, I'd
ReplyDeletelike to shoot you an e-mail. I've
got some suggestions for your blog you might
be interested in hearing. Either way, great website and I look forward to
seeing it improve over time.
Take a look at my page ; Child Custody attorney