Na
Elizabeth John
NTOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes ‘Dully
Sykes’ amaeachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Utamu’ amabao
unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Dully
alisema wimbo huo kawashirikisha wakali wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum’ na Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’ ambao anaamini wamefanya vizuri katika
wimbo huo.
“Niliamua kuwashirikisha wasanii hao kwasababu wanafanya
vizuri na wanakubalika katika ‘game’, naamini uwepo wao utakuwa wa mafanikio
makubwa kwangu pamoja na burudani kwa mashabiki wa muziki huo,” anasema Dully.
Anasema wimbo huo umeanza kuonekana katika vituo mbalimbali
vya redio wiki hii, anawaomba mashabiki wake wampokee vizuri na kwamba wasikae
mbali nay eye kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia.
Mbali na kutaka kutoka na kibao hicho, Dully alishawahi
kutamba na nyimbo zake kama Mtoto wa Kariakoo, Dhahabu na nyinginezo ambazo
zilimtambulisha na kufanya vizuri katika muziki wa bongo fleva.
No comments:
Post a Comment