Sajuki nyakati za kuugua kwake, akiwa na mkewe Wastara (Picha kwa Hisani ya Global Publishers)
Sajuki kabla ya kuanza kuumwa
DAR ES SALAAM, Tanzania
Katibu
wa Baraza la Filamu Tanzania
(TAFF), Wilson Makubi, amethibitisha kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa
akisubiriwa apate nafuu ili Serikali ya Tanzania
igharamie safari na matibabu yake nchini India
MSANII nyota wa filamu Tanzania, Juma Kilowoko, ‘Sajuki,’ amefariki dunia saa moja asubuhi ya leo, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa.
Sajuki
aalifikishwa hospitalini hapo mwishoni mwa Desemba 2012, alikofikishwa akitokea
Amana, alikokuwa akipata matibabu mbaada ya kuanguka jukwaani jijini Arusha,
alipopanda kutaka kusalimia mashabiki wake ikiwa ni harakati za kutafuta fedha michango
ya pesa za kumpeleka tena India
kupata matibabu.
Katibu
wa Baraza la Filamu Tanzania
(TAFF), Wilson Makubi, amethibitisha kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa
akisubiriwa apate nafuu ili Serikali ya Tanzania
igharamie safari na matibabu yake nchini India.
Makubi
alisema kuwa, maandalizi ya msiba huo yatatangazwa baada ya wahusika na wadau
kukukutana, huku akiwataka mashabiki wa sanaa na msanii huyo kwa ujumla kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki cha maandalizi ya mazishio yake.
Kabla
na baada ya kuifika India
kwa matibabu, Sajuki aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini,
ambapo aliporejea alionekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.
Kifo
cha Sajuki kinafanya muendelezo wa vifo vya wasanii nguli wa filamu na muziki
ulioanzia mwaka uliopita, ambapo wakali kama Steven Kanumba, John Maganga,
Mlopelo, Sharo Milionea, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ walifariki kwa nyakati
tofauti kutokana na maradhi na ajali.
Mchakato wa mazishi ya Sajuki unafanyika Tabata, jijini Dar es Salaam. MUNGU ailaze ROHO ya marehemu SAJUKI mahali pema PEPONI. Ameen.
No comments:
Post a Comment