LONDON, England
Wenger Mfaransa aliyeratibu
na kukaribia kupata saini ya pili ya mkopo ya nahodha wake wa zamani Thiery
Henry, amekiri rasmi kushindwa kwa jaribio hilo na sasa wameachana na nia ya
kumkopa Henry kutoa New York Red Bulls
WAKATI Washika Bunduki
wakikabwa koo na kulazimishwa sarte ya bao 1-1 na Southamton, kocha wa Arsenal,
Arsene Wenger amekiri rasmi kushindwa kwa jaribio lake la kumchukua kwa mkopo
nahodha wa zamani wa klabu hiyo Thierry Henry.
Mwishoni mwa Desemba, Gunners ilikuwa
na matumaini makubwa ya kupata saini ya mkopo ya mpachika mabao anayeshikilia rekodi
ya klabu hiyo, Henry, 35, akitokea klabu yake ya New York Red Bulls ya Marekani
katika usajili wa majira ya baridi ulioanza Januari 1.
Lakini Wenger alisema: “Yeye
hayuko tayari na pia hajarejea kutoka mapumzikoni kwa vyovyote. Kwa sasa hatuna
tena muda wa kushughulikia hilo.”
Jaribio hili linaloshindwa
rasmi ni la pili kwa Wenger kumtwaa kwa mkopo Henry, ambaye anashikilia rekodi
ya kuifungia Gunners mabao 228 katika mechi 337 alizocheza.
Henry ilionekana kama
aliyekaribia kumalizana na Gunners – huku akichangia kukubali nyongeza ya
mkataba mpya wa kubaki Emirates kwa mshambuliaji Theo Walcott.
Akizungumzia mechi ya sare ya
1-1 na Southampton, Wenger alisema kikosi chake kilistahili kupoteza pointi
mbili na kwamba kuna kila sababu ya kuangalia njia mbadala za kukiimarisha
kikosi katika usajili wa Januari.
Na wakati alipoonekana kutaka
kujiimarisha Januria hii na kuulizwa kama anaweza jkufanya usajili wowote, Wenger
alisema: “Ndiyo, nitakuwa kazini.
“Tutaangalia kila kona, kila
mahali, tumeamua kuwa wazi kabisa. Tunahitaji kuongeza nguvu ya kikosi chetu,”
alitamba Wenger, anayehaha kwa misimu minane sasa kusaka taji bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment