Jezi ya Mario Balotelli akiwa na klabu ya AC Milan ambayo ina namba 45
Mario Balotelli akimgaragaza kipa kwa mara ya kwanza tangu atue Milan akitokea Man City
Balotelli akionesha jezi yake mpya baada ya kukabidhiwa alipojiunga na Milan akitokea Man City
MILAN,
Italia
NYOTA wa kimataifa wa Italia, Mario Balotelli amefungua
mdomo kwa mara ya kwanza kuuzungumzia uhamisho wake kurejea San Siro, akisema amefanya
hivyo hiyo ili kuokoa soka lake baada ya kupoteza muelekeo akiwa na Manchester City.
"Sikuuanza vema huu msimu nikiwa na Man City,
hivyo nimekuja hapa Milan kufufua soka langu na
kuhakikisha nafanya vema tena," alisema Balotelli nyota wa zamani wa Inter
Milan.
Balotelli alikamilisdha uhamisho uliomrejesha San Siro
yaliko makao ya klabu hizo hasimu kwa usajili ulioigharimu Rossonerri karibu
dola za Kimarekani milioni 30.
"Mimi nilikuwa nataka sana kuichezea AC Milan kwa muda mrefu tu, lakini
nilikuwa katika timu nyingine. Wakati nafasi kama
hii inapokuja kwangu, napaswa kuitumia. Nina matumaini Milan inaweza kurejea kuwa moja ya klabu
kubwa tena."
Maisha ya Balotelli Etihad yaliko makazi ya Man City
yaliyajaa vituko na mikasa, huku mmiliki wa klabu hiyo Sheikh Mansour Al Nahyan
na kocha Roberto Mancini wakimvumilia na kuamini angebadilika bila mafanikio.
…..SuperSport.com…..
No comments:
Post a Comment