Na Bryceson Mathias
‘Mzazi Muongo kwa Wanaye huandaa Watoto Jeuri’.
Watendaji wa wizara ya elimu na ufundi; ambao kila mara ndio wanaomsaidia Rais Jakaya Kikwete, wanaweza kutafsirika kama wazazi waongo ambao wanaweza kuandaa watoto jeuri kama hawatekelezi na kufuatilia ahadi za Rais alizoahidi ili zitimizwe.
Katika kuukaribisha mwaka huu 2013 kwenye viwaja vya mnazi mmoja, Rais Jakaya Kikwete aliahidi ifikapo Januari 2013, ataajiiri Walimu 28,000.
Labda mimi nimekosea sikuelewa, labda Januari aliyoikusudia Rais ilikuwa si ya Mwaka huu 2013 pengine ni Januari ya mwaka 2014.
Kama Rais alimaanisha Januari 2013 bado hajabadili Kauli yake hivyo watendaji wantakiwa kumkubusha Rais ahadi yake ya Mnazi mmoja akiukaribisha mwaka huu, ambapo kuusindikiza 2012 uende na kuuleta haraka 2013 aliwaahidi watanzania Neema hiyo.
Siamini kabisa kwamba Rais anasubiri Januari nyingine au alikuwa anawaliwaza Walimu waliohitimu, Wazazi na Walezi wa Wanafunzi waliowalipia ada wanafunzi hao vyuoni! Au Wanafunzi na Walimu wenye mzigo mkubwa wa kufundisha la hasha!!.
Kwa mtazamo wangu nawauliza watendaji hao maswali mawili. Mosi hivi wanafahamu kwamba kuna walimu huko Wilayani, Kweye Tarafa, Kata, Vijijijini na kwenye vitongoji kuna Walimu wenye Mzigo Mkubwa kiasi kwamba wafike mahali wameelemewa?.
Pili; wanaelewa kuwa kuna wanafunzi hawana walimu kabisa wa kuweza wa kuweza kuwatoa mahali walipofinyangwa a ujinga wa kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu?
Kama watendaji wangeelewa maswali hayo; Basi wasingebweteka kwa ukimya wakiangalia na kunywa chai za Jamu na Mafuta ya ‘Blue Band’ wangechangamkia kwa bidii ahadi ya Rais aliyoahidi akiukaribisha mwaka mpya kuhusu ajiira hizo 28,000 ambazo zingewapa ahueni walimu wenye mzigo mkubwa.
Kama wangechamkia ahadi hiyo, Wanafunzi wasio na walimu kwa upande wao wangeondoka na ukosefu wa walimu, jamboa ambalo lingeliwafanya wapate elimu kwa kiwango kinachohitajika, tofauto na walivyo sasa kubaki wanacheza kwenye vumbi na kuharibu nguo, kuuza Ice au maandazi ya walimu.
Pamoja na kuwepo kwa Tatizo la Mitaala lakini pia tunatakiwa kujiuliza Je, wapo walimu wenye uwezo wa kufundisha aMiaala hiyo? maana kuwa na Mitaala ni Jamb moja na kuwa na walimu wenye uwezo wa kufundisha mitaala hiyo ni jambo lingine.
Ni heri kuwa na walimu wachache watakaolipwa vizuri kutokana na ujuzi na kujituma kwa katika kuwajibika kufundisha kwa mustakabali wa Taifa hili na vizazi vijavyo, kuliko kuwa na walimu wengi wanaoshinda wanafuma vitambaa ofisini huku wakizalisha Taaifa la wafu wa Elimu.
Hivi sasa mashuleni, tunao walimu ambao wanachagua masomo rahisi ndiyo wanayotaka wafundishe lakini masomo magumu hawataki kutokana na kutokuwa na uwezo na hiki ni kielelezo kinachootuonesha kwamba Taaluma yao baadhi ya Walimu ni ndogo (Poor).
Aidha hali ya baadhi ya walimu kuogopa masomo, inanifanya nimtaka Rais awalazimishe mawaziri husika wafanye mapitio ya Ikama ya Walimu kila Mahala pa Kazi ili kubaini kwamba, pamoja na tatizo Mitaala, huenda pia kuna sintofahamu ya Walimu wasioandaliwa vizuri ambao hawana uwezo wa kufundisha na hivyo wanajichukula mishahara ya bure.
Mbali ya kupokea mishahara,yawezekana Taaluma zao hazikidhi ukamilifuwa kuwafanya wanafunzi wasomeshwe kimitaala, lakini pengine hata wabunga kama James Mbatia anapoonesha udhaifu wa Mitaala, peng dhaifu ndine walimu wengine hata kuitumia kwao ni kumpigia Mbuzi Gitaa.
0715-933308
hongereni sana; Habari yenu ya 'JK; Ziko wapi zile ajira za Walimu 28,000?'ya 13.2.2013, imesaidia sana kuwasukuma Rais, Mawaziri na watendaji wa Elimu, Mafunzo na ufundi kutangaza ajira hizo jana 14.2.2013.
ReplyDeletetunampongeza sana mwandishi huyu, kila anachoandika kinavutia na kuwasukuma watendaji hata anapoandika kwenye Tanzania Daaima.
viongozi na wahariri wake tunaomba mumlinde na kumpongeza
Juma Athumani Kigoma