Bryceson Mathias
IMEBAINIKA kwamba, Amani Tanzania, inatafsiriwa tofauti na inavyosemwa na watu walio wengi, na hasa kwa wanasiasa wasiojua tafsiri halisi ya Amani, ambao mtaji wao mkubwa kila siku ni tamaa ya kujirundikia Rasilimali, Vyeo na Madaraka.
Mtu moja alisema hivi, yeye anakuwa na amani kama Akili yake imetulia, huku akiwa amevaa, ana mahali pa kulala na Chakula!. Lakini mbishani wake alikanusha na kusema, iwapo tunashuhudia mauaji, migomo na mambo mengi yanayoashiria kukosekana kwa amani! Tutasemaje, tuna Amani?
Kimsingi hatuwezi kujivuna kuwa sisi ni kisiwa cha Amani wakati kuna watu wana Njaa + Madeni +Uchumi duni, kiasi cha baadhi yao kula Mizizi, Matunda Pori, Wadudu kama kumbikumbi, Mboga za Majani ya miti visivyo rasmi.
Kwa jinsi ilivyo sasa, Amani ya nchi yetu imetoweka na kilichobaki ni utulivu tu na kama tusipochukua hatua za dhati kukomesha vurugu zilizopo, hata huo utulivu tutaupoteza na kujikuta umepotelea mbali, na tutakapoanza kuutafuta tutaukuta Amani yake ina majereha, na pengine imezeeka kiasi cha kufa.
Mara nyingi nashangaa kusikia Polisi wanasema, maandamo fulani yamezuiwa kwa sababu yanahataharisha Amani!. Je wanaohatarisha amani hiyo, ni nani kama si watawala wa Fikra za kisiasa, wenye nia ya kujipatia Uchumi wa Kifisadi na kudhani walio vijijini ni wajinga wasiojua kitu?.
Kama Kiongozi wa Wilaya, Tarafa, Kata, Kijiji na Mtaa; kwa MfanoMkurugenzi au Mkuu wa Wilaya, Diwani, Mtendaji Kata, Mtendaji wa Kijiji wanaweza kwenda Vijijini wakaacha kuchagua Wajumbe biala taratibu si kuwafanya wajinga?
Mwanaharakati mmoja alisema Tanzania hamna amani kwa sababu nyingi; Hela yetu haina thamani, Polisi Inawakandamiza wananchi wanapotaka kupata haki zao, Wananchi wanyimwa haki zao kwa Mkusudi, Mahakama kwa namna fulani hazitendi haki hasa ucheleweshaji wa Kesi.
Pia alisema, Hajawahi kuona matokeo mabovu ya kidato cha nne kama ya mwaka 2012, ambapo alisema watawala hawajali na kwa ujumla wanachukulia liwalo na liwe hata kama uhai wa watu uko hatarini.
Katika hitimisho alidai, Tanzania hamna amani imetoweka na kilichobaki ni utulivu tu na kama tusipochukua hatua hata huo utulivu tutaupoteza.
Aliongeza, Amani ipo midomoni mwa wana siasa na viongozi wasio makini; wanaojinadi kuhubiri Amani kumbe nyuma ya Pazia wanahubiri mafarakano na hila za kutekana na kupeana vilema vya maisha na vifo.
Alinena; akisema uwepo wa Amani Tanzania, ni sawa na kuulizia Tende na Halua kwa Mchungaji au kuuliza Divai na Mkate wa Roho Mtakatifu kwa Shekhe! Kutoweka kwa Amani nchini ni dhana halisi inayosheheni ukweli pasi na shaka.
Kama Sensa tu ya Makazi imesababisha mitafaruku ambayo hapo awali haikuwepo. Je sisi leo tumlaumu Nani? Inawezekana Amani umebaki ni Msemo wa Mazoea kwa wanasiasa, lakini si jambo muhimu la kuwa mbegu njema yenye matunda mazuri kwa Taifa.
Biblia Wafilipi 4:8-9 inasema” Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo”.
0715933308
No comments:
Post a Comment