Bondia Nathan Cleverly kushoto, akipambana kutetea ubingwa wake wa WBO dhidi ya Robin Krasniqi.
WEMBLEY, London
Bingwa huyo wa dunia wa WBO uzani wa ‘light’ ametetea mkanda wake huo kwa mara ya tano baada ya ushindi wake wa pointi dhidi ya Krasniqi, ushindi ambao ni hatua kubwa kuelekea pambano la ndoto yake dhidi ya Bernard Hopkins
BONDIA Nathan Cleverly amethibitisha uhatari wake ulingoni
na kuwa mmoja wa mabondia wakubwa katika ulimwengu wa masumbwi baada ya
kumshinda mpinzani wake Robin Krasniqi katika pambano lililofanyika Wembley
Arena mwishoni mwa wiki.
Bingwa huyo wa dunia wa WBO uzani wa ‘light’ ametetea mkanda
wake huo kwa mara ya tano baada ya ushindi wake wa pointi dhidi ya Krasniqi,
ushindi ambao ni hatua kubwa kuelekea pambano la ndoto yake dhidi ya Bernard
Hopkins.
Akizungumzia pambano na matokeo, Cleverly alisema: “Nadhani
sasa niko tayari. Mimi bado najifunza hatua kwa hatua, lakini kujiunga na ngumi
za uzito wa juu ni jambo ambalo nililokuwa nikilitaka.
“Tutaona kama nitaweza kuzalisha matokeo mazuri zaidi. Naamini
naweza.”
Cleverly katika pambano hilo alipoteza raundi ya kwanza
pekee, baada ya kupewa alama chache na majaji kulinganisha na mpinzani wake Krasniqi.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani, alifanya kazi ya ziada
kuibuka na usjhindi huio wa pointi, na mara kadhaa aliwekwa majaribuni kiasi
cha wengi kudhani Cleverly angerefusha rekodi yake ya kutopigwa na kufikia
madpambano 26.
Kwa ushindi huo, sasa Clev, 26, anakaribia kutimiza ndoto ya
kuumana na nyota machachari wa mchezo huo Hopkins, ambaye aliliangalia pambano
la hasimu wake kwa njia ya televisheni akiwa nyumbani kwao Marekani.
The Sun



No comments:
Post a Comment