BARCELONA, Hispania
"Puyol hatokuwa tayari kwa mchezo wa Jumanne jijini
Munich na hatujui kama ataweza kuiwahi mechi ya marudiano (Mei 1). Mascherano
anaendelea vizuri, lakini pia hatujui kama ataiwahi mechi ya marudiano"
NYOTA wawili wa safu ya ulinzi wa FC Barcelona, Carles Puyol
na Javier Mascherano watalazimika kulikosa pambano la kesho Jumanne la nusu
fainali ya amabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Kocha Msaidizi wa Barca Jordi
Roura amethibitisha.
Puyol, nahodha wa kikosi hicho, amefanyiwa upasuaji wa
kifundo cha mguu alichoumia mwezi uliopita, huku Mascherano aakivunjika mifupa
midogo katika mechi ya sare ya 2-2 dhidi ya Paris St Germain iliyopigwa Aprili
2.
"Puyol hatokuwa tayari kwa mchezo wa Jumanne jijini Munich
na hatujui kama ataweza kuiwahi mechi ya marudiano (Mei 1), itategemea ni kwa
namna gani atapona haraka, lakini pia itategemea na maamuzi ya daktari," alisema
Roura.
"Mascherano anaendelea vizuri, lakini pia hatujui kama
ataiwahi mechi ya marudiano," aliongeza Roura anayekaimu nafasi ya kocha
Tito Vilanova anayemaliza muda wa mapumziko kutokana na operesheni ya kansa ya
tezi.
Barca, inayofukuzia ubingwa wa tatu wa Ulkaya katika misimu
mitano, ina machaguo kadhaa katika kumpata mshirika wa Gerard Pique katika
ulinzi wa kati, iakiwamo beki wa pembeni Adriano, kinda wa kikosi cha vijana Marc
Bartra na viungo Alex Song na Sergio Busquets.
Eric Abidal, ambaye ameanza kukitumikia kikopsi cha Barca
hivi karibu akipona kutoka katika upandikizaji wa Ini, anaweza kuwa chagu
jingine la Roura, ingawa anahitaji muda zaidi kabla ya kurejea katika
mikikimikiki ya mabingwa Ulaya.
"Kimsingi Abidal tunapaswa kumchukulia hatua kwa hatua.
Ni kawaida kwamba yeye ameonesha nia ya kucheza, kama ilivyo kwa wachezaji
wenzake. Amejifua vya kutosha, amefanya mambo makubwa na yuko fiti kama wakati
mwingine."
Aidha, nyota wa utikisaji nyavu wa kikosi hicho, Lionel
Messi ameripotiwa kuwa yu tayari kwa mpambano wa kesho, baada ya kuwa shakani
kutokana na kuumia katika mechi dhidi ya PSG.
"Messi yuko katika hali nzuri," alisema Roura.
"Amerejea kazini na kikosi huku akioenesha utayari utokanao na kupona kwa
haraka na naamini atafanya kila liwezekanalo kuwa fiti zaidi."



No comments:
Post a Comment