HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 20, 2013

Hospitali ya Dodoma ikomeshe Rushwa na Wizi wa Watoto Wachanga


Na Bryceson Mathias
 
'Lisemwalo lipo, kama halipo liko njiani linakuja’
 
KAMA si Menejimenti ya Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital), basi Serikali yenyewe kwa ujumla wake, ikomeshe tuhuma za kuwepo rushwa kwa Wajawazito wanaojifungua, na Wizi wa watoto wachanga wakati wa upasuaji; Jambo ambalo linaitia aibu Hospitali hiyo na Taifa.
 
Wajawazito walio wengi na wazazi waliojifungua salama hospitalini hapo na kuomba wasitajwe, wamelalamikia kuwepo kwa rushwa iliyokithiri wanapojifungua, ikidaiwa wanombwa kutoa kati ya Sh.60,000 – 300,000/-  kulingana na ukubwa wa tatizo;  na wanaojifungua kwa upasuaji, wamekuwa wakiibiwa watoto au kubadilishiwa waliokufa.
 
Kashfa kama hiyo na nyinginezo, awali iliiandama sana Hospitali ya Mwanyamala Dar es salaam, lakini sasa meota na kumea Dodoma, vilipo vikao vya Bunge, jambo ambalo ni aibu kwa Menejimenti ya Hospitali hiyo, Watalaam, Watendaji na Serikali nzima kwa ujumla.
 
Jumatano, Aprili 17, mwaka huu, Amana Amosi Mbigili na Mumewe Isaya Nyembele, walionja Uchungu wa Uzazi ambapo baada ya Amana kujaliwa mtoto kwa upasuaji, alifanyiwa njama abadilishiwe mtoto liyekufa, ambapo kwa ujasiri Amana aling’ang’ana kuwa arudishiwe mwanae hai aliyebebwa na Muuguzi.
 
Pamoja na Kaimu Mganga Mkuu Zainab Chaula kukiri ni kweli tukio hilo lilitokea lakini limenukuliwa tofauti, kwa nini nduguze wpelekwe chumba cha maiti wakakabidhiwe mtoto aliyekufa? Kwa nini mtoto awekwe mbali na Mzazi wake? Kwa nini mtoto apatikane baada ya malumbano  ya wazazi kutishia kumuona Mganga Mkuu wa Mkoa?
 
Bado tuna kumbukumbu miaka ya nyuma, ambapo Hospitali hii ilikumbwa na Kashfa ya kuwa na Dakitari aliyekuwa na vyeti na, Serikali ikamuajiri akalipwa Kodi ya walalahoi.
 
Bado hatujasahau walala hai waliposababisha watalaam Mhimbili walimfanyie mtu upasuaji wa kichwa badala ya mguu. Ndiyo maana tunasikiti na kulia tunapoona Kiti cha Spika na Serikali Sikivu, vinawasikia na kuwakumbatia baadhi ya Wabunge wavuta Bangi wanaotukana Matusi bungeni, wakati mashamba ya Bange yanatomwa, ni Jinai.
 
Kwa ufupi kilichomtokea Amana aliyefanyiwa upasuaji akiwa kitandani alidai hivi,
 
“Nlishangazwa na kitendo cha Muuguzi kunilaza chumba tofauti na mwanangu; nilipomuuliza mtoto  akanijibu alishafariki, kitendo ambacho sikuridhika nacho, kutokana na kuona mtoto mwingine akipitishwa na kuingizwa chumba kingine akiwa amefungwa na nguo nilizofika nazo hospitalini akiwa hai.
 
“Nilikuwa hoi na maumivu makali, lakini nilikuwa na ufahamu. Nilipoanza kulalamika kwa sauti, ndipo wakaamua kuniletea mtoto wangu akiwa hai, kitendo kilichonifanya nilie kwa furaha baada ya kumpata mwanangu. Si kweli kwamba walichanganya watoto, walitaka kuniibia makusudi.
 
Kama walichanganya watoto, mbona sikumuona mama wa mtoto marehemu? Mungu ndiye anajua, mimi namshukuru,’’ alisema Amana.
 
“Hawawezi kuniuliza lolote! Hebu hilo liwe funz kwaoo, lakini ni vema Serikali ikomesha madhaifu haya, maana yanaitia aibu Taifa na viongozi wake. Mke wangu bado ana maumivu makali, hivyo tunaendelea kumuuguzi na bado amelazwa kama unavyoona, na mimi sichezi mbali”.alisema Nyembele.
 
 
Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Ezekiel Mpuya ambaye hakuwepo siku hiyo alipohojiwa na Mwandishi alikiri kusikia Malalamiko hayo na atayafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa karibu tuhuma ya rushwa iliyokithiri kwa wajawazito wakati wa kujifungua, ili wachukuliwa hatua Kali.
Ni rai yangu Hospitali ya Dodoma ikomeshe Rushwa na Wizi wa Watoto Wachanga.
 

No comments:

Post a Comment

Pages