HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 15, 2013

Pinda; Utalia tena lini bungeni, Utekaji na kuteswa kwa wananchi?


Na Bryceson Mathias
 
IJUMAA, 29 Januari 2009, WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, alizua simanzi bungeni baada ya kububujikwa machozi wakati akitoa ufafanuzi wa kauli yake ya kutaka wanaoua albino na vikongwe, na na wenyewe wauawe.

Pinda ambaye alikuwa akizungumza kwa uangalifu juuu ya tukio hilo, alikuwa akitoa ufafanuzi wa kauli yake hiyo, ambapo alianza kudondosha machozi akielezea jinsi albino walivyofanyiwa ukatili na wanaowaua kwa sababu tu ya kutaka kutumia viungo vyao kusaka utajiri.

Hatua hiyo ya kihistoria kwa Pinda kutokwa na machozi mbele ya wabunge akitoa maelezo yake, ilisababisha hamasa iliyoonekana na wabunge kabla hajaanza kujibu swali hilo kuyeyuka, huku ikiwafanya baadhi kupata simanzi na wengine kutoamini walichokiona.

Kilichosababisha Pinda afikie hatua ya kububujikwa machozi ndani ya Bunge hata kusababisha alazimike kuvua miwani aliyokuwa ameivaa na kuyafuta, ni swali aliloulizwa na Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohammed (CUF) ambaye pia alikuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Katika swali lake hilo, Hamad alimtaka Pinda atoe ufafanuzi kuhusu kauli aliyoitoa akiwa ziarani mkoani Tabora ambako aliwataka wananchi kuwaua mara moja wale wote watakaokamatwa wakijaribu au kuwaua albino.

Alipojibu swali hilo alionesha hisia za kuguswa na matukio yaliyowakumba albino, ambapo alisema ni jambo linaloumiza sana moyo iwapo utabahatika kusikiliza maelezo yanayotolewa na albino ambao wamepoteza viungo kutokana na kukatwa na watu wanaoua albino.

"Nchi yetu tumekuwa na heshima sana, lakini mauaji haya yametutia doa. Katika kipindi cha miaka mitano, jumla ya vikongwe waliouawa ni 2,866, hii ina maana kwamba, kwa kila mwaka vikongwe 537 huuawa kikatili kwa mapanga na nyundo kwa sababu za kishirikina. 

“Wakati hali ikiwa hivyo kwa vikongwe, mwaka 2006, mauaji ya albino nayo yakaanza, wenzetu hawa wanauawa kwa sababu tu wauaji wanatafuta viungo vyao wakasake utajiri, inasikitisha sana, inauma sana,” alisema Pnda kwa kwa simanzi.

Hivi karibuni kumekuwa na utekeji na uteswaji wa wananchi na hasa wandishi wa habari akiwemo, Mwandishi wa Channel Ten Daudi Mwangosi aliyesambaratishwa na Bomu tumboni na kufa, jambo ambalo limewaumiza mioyo watanzania na kuona kama hawana msaada.

Wengine ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalumu Kibanda aliyeumizwa vibaya kiasi cha kutobolewa Jicho lake, na wandishi wengine walikutwa na adha mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka.

Ni hakika na furaha yangu kwamba, kama machozi ya panda yangetoka tena bungeni kama yalivyotoka Ijumaa, 29 Januari 2009 na kuwagusa wabunge wote wasiamini kilichotokea, Watekaji, Watesaji na Wauaji wa wananchi na waandishi wasio na hatia, nao wangelia na kuona kitendo hicho ni kibaya ili waache kisiligawe na kuliangamiza Taifa.

Kimsingi Pinda alilazimika awaombe radhi Watanzania kwa kauli yake kutokana na tafsiri mbalimbali tofauti zilizojiri wakati huo kinyume na matarajio ya wengi nay eye mwenyewe kuhusu Kauli yake hiyo, iwapo ingeweza kuzua mtafaruku na hisia tofauti.

Matukio yaliyotokea bungeni hivi karibu ambapo Mwigulu Mchemba na Tundu Lissu walitunishiana misuli ya Kauli bungeni, yalihitaji buujiko la machozi hususani lile la kububujikwa machozi kwa Pinda linaweza kugeuka na kuwa suluhisho la kitendawili hicho kigumu kati ya Kambi ya Upinzani bungeni na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


0715-399908.

No comments:

Post a Comment

Pages