Profesa Lipumba, akiangalia ukuta uliojengwa na wananchi wa Kijiji cha Kigombe mkoani Tanga, mara baada ya kuuzindiwa, kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mzee Said.
Mwandishi Wetu, Tanga
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa maarufu kwa viwanda nchini lakini hivi saa hali ya kimaendeleo katika mkoa huo imekuwa mbaya.
Kauli hiyo ameitoa leo mjini hapa alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu maendeleo ya uchumi kwa Mkoa wa Tanga katika kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kwa kushirikiana Taasisi ya Maendeleo ya demokrasi kwa vyama vya siasa ya nchini Denmark (DIPD).
Profesa Lipumba alisema kuwa hakuna haki bila kuwa na maendeleo yanamgusa mwananchi wa kawaida.
Alisema Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuwa na rasimali nyingi ikiwemo zao la Mkonge ambalo kwa sasa limekosa msukomo hali inayochangia umaskini kwa wananchi wa mkoa huo.
"Pamoja na Tanga kuwa na fursa nyingi za kiuchumi lakini bado kadri siku zinavyokwenda umaskini umekuwa ukiwatesa wananchi. Viwanda vilikuwa zaidi ya 70 lakini sasa hakuna hata kimoja kinachofanya kazi huku zao la mkonge lilikosa msukumo wa makusudi kwa wananchi wake.
"Katika soko la dunia inaonyesha kuwa Tanga ilikuwa ikizalisha tani 234,000 kwa mwaka lakini sasa mkonge umeporomoka na kufikia tani 25,000 tu hali ambayo imekuwa ikiongeza umaskini kila kukicha. Kama kungekuwa na msukumo wa makusudi wa kufufu zao hili ni wazi Tanga ingekuwa imepaa kimaendelo kwa wananchi wake kutokana na kuwa na kila aina ya rasilimali zikiwemo za matunda na mbogamboga," alisema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi duniani, alisema ili kuweza kufikia malengo ya mkoa huo kuweza kupambana na umaskini ni lazima serikali ikubali kwa kufanya uwekezaji hasa katika kufungua bandari ya Tanga ambayo ni lango kuu la kiuchumi.
Alisema Bandari ya Tanga imekuwa haitumiki ipasavyo hali inawechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa umaskini na hazorotesha harakati za mkoa na wananchi kwa ujumla.
"Bandari ya Tanga, zao la mkonge pamoja na kukosekana kwa msukumo wa kuimarisha sekta ya elimu ni moja ya masuala yanayoufanya mkoa huu kuzidi kurudi nyuma kiuchumi pamoja na wananchi wake,” alisema Profesa Lipumba.
TANGA SISI NI WELEWA NA SI VIPOFU!! ANAMAANA GANI KUSEMA " KULIKUWA NA VIWANDA ZAIDI YA 70 SASA HAKUNA HATA KIMOJA"????? !!!!. JAMA HUU NI UONGO WA MCHANA KWEUPE TUNAVIWANDA VIDOGO 214, VIWANDA VYA KATI 30 NA VIWANDA VIKUBWA 3. NA HATA FOMA IMEAANZA KAZI.NA SWALA LA MKONGE PROF. ANAJUA FIKA KWANINI ULIKUFA NA SASA NDO JITIHADA ZINAFANYIKA ZA KUFUFUA, ULAYA WALIAMUA KUTUMIA MANILA BADALA YA KATANI SASA TUNGEZALISHA TUTUPE BARABARANI?HATA HIVYO WALIOKUWA WANAFANYA KAZI KWENYE MASHAMBA YA MKONGE SI WAZAWA WA TANGA MTEMBEZENI AANGALIE MABAKI YA KIZAZI KILICHOKO KWENYE MASHAMBA AU KATIKA VIJIJI VINAVYOZUNGUKA MASHAMBA HAYO.PROF. YUKO TAYALI KWENDA KULETA WARUNDI, WANAYAMWEZI , WABENA , WASAFA NA WANYAKYUSA WAJE WAFANYE KAZI KWENYE MASHAMBA YA MKONGE AU ANATAKA SERIKALI IINGIE KWENYE KILIMO CHA MKONGE? NA KUNATATIZO GANI PROF. KUJA KUWEKEZA TANGA KWENYE MKONGE?. pALE KIJIJINI KWEKE MH:PROF. GOROFA LINATAKA KUANGUKA MZEE MBONA HUJA WEKEZA PALE AU NAPO MNALIMA MKONGE? JAMANI WASHAURI MPENI UKWELI PROF. KABLA HAJAHUTUBIA HADHARA MAANA MAMBO KAMA HAYA YANA MSHUSHA HADI PROF.
ReplyDelete