WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema hafla ya nne ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itafanyika Aprili 13, 2026 kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri Mkenda, tuzo za mwaka huu zimehusisha nyanja nne za fasihi ambazo ni riwaya, hadithi za watoto, tamthiliya na ushairi.
"Tunaendelea kukuza Kiswahili, kuendeleza vipaji vya uandishi bunifu, kulinda historia na utamaduni wa taifa na kuongeza hifadhi ya vitabu katika maktaba ndio malengo hasa ya tuzo hii," amesema Waziri Mkenda.
Sambamba na hayo Waziri Mkenda amebainisha kwamba mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Mshairi maarufu duniani Abdilatif Abdallah, mwenye asili ya Afrika Mashariki, ambaye aliwahi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 15.
Hafla hiyo itatanguliwa na mjadala wa kitaaluma utakaoshirikisha waandishi bunifu wa Tanzania na wageni mashuhuri kutoka Uganda na Rwanda.


.jpeg)






No comments:
Post a Comment