LONDON, England
Gazeti la The Sun lilifichua mpango wa bosi mpya anayekaribia kushika hatamu klabuni Allianz Arena yaliko makazi ya Bayern, Pep Guardiola wa kuchuana na Madrid na PSG katika vita ya kupata saini yam kali huyo
MWENYEKITI wa klabu ya Tottenham Hotspur ya jijini hapa,
Daniel Levy, ametaja dau la pauni milioni 100 ndilo linaloweza kumng’oa winga wake
hatari Gareth Bale, klabuni White Hart Lane.
Levy amelitaja dau hilo rekodi ya dunia kupata saini ya
winga huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 27, akimini ni sahihi kwa
mkali wake huyo kutua popote miongoni mwa klabu zinazomuwinda.
Anaamini nyota huyo anayewindwa na klabu kongwe na tajiri
duniani za Bayern Munich ya Ujerumani, Real Madrid ya Hispania na Paris
Saint-Germain ya Ufaransa, ana kiwango kikali kitakachoongezeka zaidi, pindi
atakapotua katika klabu hizo.
Gazeti la The Sun lilifichua mpango wa bosi mpya
anayekaribia kushika hatamu klabuni Allianz Arena yaliko makazi ya Bayern, Pep
Guardiola wa kuchuana na Madrid na PSG katika vita ya kupata saini yam kali
huyo.
Lakini Levy anataka kubaki na nyota huyo kusaidia harakati
za klabu yake, angalau kwa mwaka mmoja zaidi.
Kushindwa kushika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi
Kuu ya hapa kunakoweza kuipa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, kunaweza
kumsukuma Bale kutimka klabuni hapo kiangazi hiki.
The Sun



No comments:
Post a Comment