HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 02, 2013

CHELSEA KUFUZU FAINALI EUROPA LEAGUE LEO VS BASEL?


 David Luzi (katikati) akishangilia bao lake lililoipa Chelsea ushindi katika mechi ya kwanza. Kulia ni Cesar Azpilicueta na kushoto Victor Moses ambaye alifunga bao la kwanza katika ushindi huo wa mabao 2-1 dhidi ya FC Basel ya Uswisi. Timu hizo zinarudiana leo Stamford Bridge. 
Mshambuliaji Fernando Torres wa Chelsea akiruka kwanya la beki wa FC Basel. Timu hizo zinarudiana leo katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Europa League 2013.

LONDON, England 

Fainali ya Europa League mwaka huu inatarajia kupigwa kwenye dimba la Amsterdam Arena, jijini Amsterdam nchini Uholanzi, hapo Mei 15, siku 10 tu kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye dimba la Wembley jijini London, Uingereza

WAWAKILISHI pekee wa England katika michuano ya klabu barani Ulaya, Chelsea, leo wanajitupa dimba la Stamford Bridge jijini hapa, kuwaalika FC Basel ya Uswisi, katika marudiano ya nusu fainali ya Europa League.

Chelsea inahitaji sare ya aina yoyote leo kuweza kufuzu fainali ya michuano hiyo ya pili kwea ukubwa ngazi ya klabu Ulaya, baada ya kushinda mechi ya Alhamisi iliyopita, kupitia mabao ya Victor Moses na David Luiz ugenini St Jacob Park.

The Blues iliangukia katika Europa League baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa, ilikoweka rekodi ya kuwa bingwa wa kwanza kushindwa kutinga mtoano, kabla ya kushinda mechi moja baada ya yingine katika michuano hii.

Mshindi wa mechi ya Chelsea na Basel, ataumana fainali ya michuano hii na mshindi wa nusu fainali ya pili, ambapo leo Benfica itakuwa nyumbani Estadio da Luz, kuwaalika Fenerbahce ya Uturuki, inayoongoza kwa bao 1-0 ililopata katika mechi ya kwanza.

Fainali ya Europa League mwaka huu inatarajia kupigwa kwenye dimba la Amsterdam Arena, jijini Amsterdam nchini Uholanzi, hapo Mei 15, wiki moj tu kabla ya fainali ya Mabingwa Ulaya kwenye dimba la Wembley jijini London, Uingereza.

Mshambuliaji Libor Kozak wa Lazio ya Italia, ni kama tayari ametwaa Kiatu cha Dhahabu cha Europa League akiwa na mabao nane, licha ya timu yake kutolewa mashindanoni na hakuna dalili za kupitwa.

Oscar Cardozo wa Benfica, Fernando Torres wa Chelsea na Marco Streller na Fabian Schar wa FC Basel walio mashindanoni hadi sasa, kila mmoja ana mabao manne, hivyo kuhitaji mengine zaidi ya hayo katika mechi za leo na fainali ili kumpiku Mserbia huyo.

Uefa.com/Supersport.com

No comments:

Post a Comment

Pages