Majaji wa shindano la Tusker Project Fame, Ian Mbugua kushoto, Juliana Kanyomonzi, na Hermes Bariki wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kinyang'anyiro hicho
KAMPALA, Uganda
“Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ian. Yeye ni mmoja wa watu ninaofanya nao kazi pamoja Tusker Project Fame (TPF) na sio zaidi ya hapo. Namuheshimu yeye kama jaji mwenza na mtu wa familia. Tetesi hizi ni upotoshaji tu”
MKALI wa muziki Afrika Mashariki na Kati, Juliana Kanyomozi
wa Uganda ,
jana amezikana taarifa zilizozagaa kupitia mitandao ya kijamii, kuwa anajiandaa
kufunga pingu za maisha na Ian Mbugua - Jaji mwenza wa shindano la Tusker
Project Fame.
Kanyomozi (picha ndogo kulia), ametumia ukurasa wake wa Facebook kuzikana taarifa
zilizodaiwa kutoka kwa rafiki wa karibu wa Jaji Ian, ambaye ni mume wa mtu,
akimkariri jaji huyo kuwa amezama kimahusiano na anatarajia kufunga ndoa
baadaye mwaka huu.
“Habari zenu marafiki, nimeona tetesi kupitia mitandao hii
ya kijamii ikisema mengi kunihusu mimi na nimeona nivunje ukimya juu ya hilo kwa kusema kwamba
sina mpango wowote wa kufunga ndoa na Jaji Ian.
“Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ian. Yeye ni
mmoja wa watu ninaofanya nao kazi pamoja Tusker Project Fame (TPF) na sio zaidi
ya hapo. Namuheshimu yeye kama jaji mwenza na
mtu wa familia. Tetesi hizi ni upotoshaji tu,” aliandika Kanyomozi.
Mapema Jumamosi iliyopita, mitandao ya kijamii ya nchini Uganda
ilimkariri mtu aliyejiita rafiki wa karibu wa Jaji Ian akithibitisha kuwa
rafikiye huyo hafichi mahusiano yake na Juliana na kuwa wanajipanga kufunga
ndoa.
Chanzo hicho kilimkariri Jaji Ian akisema kuwa: “Siwezi
kuitoa sadaka furaha yangu, Juliana ndiye furaha yangu. Hata kama itanigharimu
kuchukiwa na kila mmoja, niko tayari kumuoa Juliana. Yeye ndiye Juliet wangu, na
mimi ndiye Romeo wake."
No comments:
Post a Comment