Na Elizabeth
John
MASHINDANO ya Wazi ya Mchezo wa Riadha, yanatarajia kuendelea kutimua vumbi Mei 25 mkoani Dodoma baada ya kufanyika wiki iliyopita mkoani Arusha na jijiji Dar es Salaam.
Mashindano
hayo ndio yatakua ya mwisho na kuwapa nafasi viongozi wa Shirikisho la Riadha
Tanzania (RT) kuchagua timu ya taifa ya vijana ambayo itaiwakilisha Tanzania
katika mashindano ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es
Salaam, Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui
alisema hayo ni mwendelezo wa mashindano yaliyofanyika wiki iliyopita ambayo
yaliudhuriwa na klabu mbalimbali.
“Lengo la mashindano hayo ni kutafuta vijana chini ya
miaka 20 kwa ajili ya kuunda timu ya Taifa ya viijana,” alisema Nyambui.
Alisema baada ya kumalizika kwa mashindano hayo,
kamati itakaa ili kuorodhesha majina ya vijana watakaoweza kuunda timu ya taifa
ya vijana chini ya miaka 20.
Alisema anawaomba wapenzi wa mchezo huo
kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuonesha ushirikiano kwa wachezaji
watakaojitokeza kushiriki katika mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment