Kikosi cha Taifa Stars
DAR ES SALAAM, Tanzania
Wakati huo huo; Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), limemteua mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania, Leslie Liunda, kuwa mtathimini wa waamuzi (referee assessor) wa mechi ya kuwania kufuzu fainali hizo za Brazil mwakani, kati ya vibonde wa kundi Cape Verde na Equatorial Guinnea
WACHEZAJI 24 wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars,’
wameingia kambini jana jioni na leo asubuhi kuanza mazoezi ya kujiandaa na
mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco itakayopigwa Juni
8, mjini Marakesh, nchini Morocco.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, nyota wote wameitikia
mwito wa kambi hiyo na kwamba jana walianza mazoezi kwenye Uwanja wa Karume,
chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen.
Alisema kuwa, kambi hiyo itaendelea kwa wiki mbili kuelekea
mechi hiyo kwenye dimba la Stade de Marrakech, ambayo kabla yake Stars itacheza
kirafiki dhidi ya Sudan jijini Adis Ababa, Ethiopia Juni 2 kama ilivyoelezwa na
Poulsen alipotangaza kikosi.
“Sisi kama TFF tumefurahishwa na mwitikio wa wachezaji,
kuwapo kwao kambini kwa wakati mmoja, kutampa kocha Poulsen wigo mpana wa
kuwanoa kujua nani na nani wako katika kiwango kizuri kupeperusha bendera ya
taifa,” alisema Wambura.
Wakati huo huo; Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), limemteua
mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania, Leslie Liunda, kuwa mtathimini wa waamuzi (referee assessor) wa mechi ya
kuwania kufuzu fainali hizo za Brazil mwakani, kati ya vibonde wa kundi Cape
Verde na Equatorial Guinnea.
No comments:
Post a Comment